Iran: Wachora katuni ‘wamkalia kooni’ Khatami kwa kupiga kura

Unawezaje kuwa “mkosaji mkuu” katika uchaguzi kwa kule tu kupiga kura yako? Labda Mohammad Khatami, Rais mwanamageuzi wa zamani wa Iran anaweza kulijibu hili.

Khatami alipiga kura kwenye uchaguzi wa bunge siku ya Ijumaa, Machi 2, 2012 akigeuka apizo ambalo yeye mwenyewe aliliweka hapo siku za nyuma ambapo kinyume na kutekelezwa kwa apizo hilo basi asingeshiriki kupiga kura: “Uhuru wa wafungwa [wa kisiasa] na kutengeneza mazingira huru kwa kila mmoja na makundi yote, serikali inayoheshimu Katiba na kutengenezwa kwa mfumo unaodhibiti upigaji kura ulio huru na wa haki.”

Kufuatia miito kutoka kwa watu wengi ya kutaka kususiwa kwa uchaguzi, wanamageuzi wengi walihuzunishwa kuona Khatami akikigeuka kiapo chake mwenyewe.

Baadae alijaribu kutetea kitendo chake hicho akieleza matumaini yake kwamba kupiga kwake kura hakukuvuruga “mshikamano wa mageuzi”. Aliripotiwa kusisitiza “hali tete” wa hali ya ndani na ya kimataifa na kutoa wito kwa kila mmoja “kuelewa hali tete iliyopo”.

Katuni nyingi za kebehi zilizochapishwa mtandaoni zinaonyesha hasira na kukatishwa tamaa na kiongozi Khatami ambaye kipindi fulani alikuwa kipenzi cha watu.

Nikahang, ambaye ni mchora katuni anayeongoza na pia mwanablogu, alichukulia kwamba Khatami alikuwa amepuuza umwagaji damu uliotokea mwaka 2009 kufuatia maandamano dhidi ya utawala ulio madarakani.

Mwanakatuni mwingine gwiji, Mana Neyestani, anaonyesha mtu anayepasua kioo kwenye kichwa cha Khatami.


Mchora katuni mwingine ambaye hakutajwa jina aliyekuwa kama mchora katuni aliyekaribishwa kwenye Khodnevis.org naye alishiriki kwenye kampeni ya “katuni za kumpinga Khatami” akiingiza mchoro huu:


Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.