· Julai, 2013

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Julai, 2013

Wanawake Watatu Wauawa katika Maandamano ya Kumtetea Morsi

  21 Julai 2013

Waandamanaji wanaomuunga mkono Morsi wameshambuliwa na mahuni huko Mansoura, tukio lililopelekea wanawake wasiopungua watatu kuuawa pamoja na makumi mawili wengine kujeruhiwa. Watumiaji wa mtandao wameonesha hisia zao kufuatia shambulio hilo.

Al Jazeera Yatuhumiwa Kutangaza “Habari za Upendeleo”

  12 Julai 2013

Al Jazeera iko kwenye wakati mgumu nchini Misri kwa kile kinachoelezwa na wengi kuwa ni "upendeleo" wake katika kutangaza habari zake wakati na baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi mnamo Julai 4. Kituo hicho cha televisheni kilichopo nchini Qatar kinatuhumiwa kuegemea upande wa wafuasi wa Muslim Brotherhood na kimegeuka kuwa mdomo wa kikundi hicho.

Misri yasema: “HAYAKUWA mapinduzi ya kijeshi”

  7 Julai 2013

Hatua ya Marekani kuingilia masuala ya ndani ya Misri - habari zinazotangazwa mashirika ya habari, hususani CNN, kuhusu siasa zinavyoendelea Misri - zilikumbana na moto jana usiku. Kung'olewa kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi baada ya kudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu madarakani kuliamsha shamra shamra nchi nzima, pamoja na vurugu kati ya wafuasi na wapinzani wa Morsi.

Misri: Wafuasi wa Morsi Wapambana na Waandamanaji Wanaompinga Morsi

  6 Julai 2013

Mapambano yaliyotarajiwa kati ya wafuasi wa Muslim Brotherhood na waandamanaji waliotaka rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi aondoke yametokea leo [June 6, 2013]. Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza na ulionekana moja kwa moja kwenye televisheni, na ulirushwa kwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya ndani na vile vya kimataifa. Watu wasiopungua 17 waliuawa na zaidi ya waandamanaji 400 wakijeruhiwa katika mapigano nchini kote Misri leo, tukio ambalo mitandao mingi ya kijamii inalielezea kama "lililotarajiwa" na "linalosikitisha."

Raia wa Misri Wamng'oa Morsi Madarakani

  4 Julai 2013

Mohamed Morsi, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Brotherhood siyo tena Rais wa Misri. Morsi ameondoshwa madarakani baada ya kutumikia kwa mwaka mmoja kama Rais mara baada ya maandamano makubwa nchini kote Misri yaliyomtaka kujiuzulu, maandamano hayo yalianza mapema mwezi Juni 30. Mkuu wa majeshi ya Misri, Generali Abdel Fattah Al Sisi, katika matangazo ya mojakwa moja dakika chache zilizo pita, alisema kuwa, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba ndiye atakayekuwa Rais mpya wa mpito na kwamba serikali ya kitaifa ya Kiteknokrasia itaundwa.

Simulizi la Video [IsiyoHalisi] ya Kukamatwa kwa Morsi

  3 Julai 2013

Video inayoonyesha kile kinachoelezwa kuwa kukamatwa kwa rais wa zamani za Misri Mohamed Morsi inatembea sana mtandaoni hivi sasa. Video hiyo hiyo iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube mnamo Mei 21, 2013 kwa kichwa cha habari "Wakati Rais Mohamed Morsi na mwanae walipokamatwa."