· Agosti, 2010

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Agosti, 2010

Tunisia: Picha ‘Zilizochakachuliwa’ ni Dalili ya Hali Halisi katika Vyombo vya Habari vya Kitaifa

Utumiaji vyombo vya habari vya kitaifa nchini Tunisia kama chombo vya kupigia propaganda ni jambo ambalo limeripotiwa vya kutosha. Ushahidi wa hivi karibuni kabisa wa utumiaji mbaya wa vyombo vya habari umewekwa bayana na wanablogu wa nchi hiyo mnamo tarehe 20 Agosti baada ya magazeti ya Le Temps na Assabah kuchapisha ripoti kuhusu taasisi ya hisani ya Zeitouna kutuma msaada wa kibinadamu wa chakula kwa waathirika wa mafuriko nchini Pakistani.

25 Agosti 2010

Moroko: Mtoto Mwanablogu Asalimia Ulimwengu

Salma alianza kublogu akiwa na umri wa miaka sita ili kuwasiliana na ndugu na marafiki. Chii ya usimamizi wa wazazi wake, mwanablogu huyu mdogo wa Moroko anapendelea kuandika hadithi fupi fupi na kuielezea dunia matukio anayokumbana nayo kila siku shuleni.

16 Agosti 2010

Mashindano ya Video: Intaneti Kama Chombo cha Kueneza Amani

Mfumo wa Intaneti umependekezwa kwa ajili ya kupata Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2010. Kama sehemu ya mjadala unaoendelea kuhusu mchango wa Intaneti katika jamii nzima ya binadamu , Condé Nast na Google Ireland wameungana na kuandaa mashindano haya ya video na mshindi atapata fursa ya kusafiri na pia video yao kuoneshwa kupitia MTV ya Italia.

15 Agosti 2010