Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Mei, 2013
Lebanon: Mwanablogu Apata Kipigo kwa Kupiga Picha
Mwanablogu wa ki-Lebanoni Habib Battah anaeleza namna alivyoshikiliwa bila hiari, akilazimishwa kufuta picha katika kamera ya simu yake na kudhalilishwa mfululizo katika posti hii inayohusiana na ripoti ya Beirut. Aliporipoti...
Wafanyakazi Wavamia Majengo ya Serikali Nchini Mauritania
Siku ya Jumanne asubuhi, Mei 28, 2013, maelfu ya vibarua, wanaolipwa ujira wao kwa kufanya kazi kwa siku, walianzisha maandamano makubwa [ar] huko Zouérat, mji mkuu wa jimbo la Tiris...
Mwandishi Habari za Kiraia wa Miaka 14 Auawa Akiripoti Mapigano Nchini Syria
Omar Qatifaan, mwanaharakati wa Habari mwenye umri wa miaka 14 ameuawa akiwa katika jitihada za kutangaza habari za mapigano kati ya vikosi vya kijeshi vinavyoiunga mkono serikali na vile vya waasi katika eneo la Daraa al-Ballad kusini mwa Sryria karibu na mpaka wa Jordan.
Saudi Arabia Yawanyonga Raia Watano wa Yemeni na Kutundika Miili Yao Hadharani
Raia watano wa Yemeni waliotiwa hatiani kwa mauaji na ujambazi walinyongwa kwa kukatwa kichwa nchini Saudi Arabia na miili yake kuanikwa hadharani huko Jizan, mji ullio kusinimagharibi mwa nchi hiyo. Picha za miili hiyo ikining'inia kwenye kamba hewani ilisambaa kwenye mtandao wa Twita na facebook kama hatua ya wa-Yemeni kupinga ukatili huo.