Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Januari, 2009
MENA: Maoni Wakati Wa Kuapishwa Obama
Tukio la kihistoria limetokea Marekani leo wakati Barack Obama alipoapishwa kuwa rais wa 44. Wakati kuungwa mkono kwa Obama kati ya Waarabu kumekuwa kukipungua katika miezi michache iliyopita kufuatia uteuzi...
Kivu Mpaka Gaza: Namna Vyombo Vya Habari Vinavyochagua Vipaumbele
Mdahalo unaodadisi ni kwa nini vita katika Mashariki ya Kongo vinapewa kipaumbele kidogo ikilinganishwa na migogoro inayotokea Mashariki ya kati. Mwandishi wa habari wa Rue89 anauliza, "ikiwa kifo cha Muisraeli mmoja ni sawa na vifo kadhaa vya Wapalestina, ni maiti ngapi za watu wa Kongo zitakazowekwa kwenye mnara wa mazishi huko Gaza?" Wanablogu wa pande zote mbili wanalichambua swala hilo.
Serikali Ya Irani Yautumia Mgogoro Wa Gaza Kukandamiza
Wakati wanablogu kadhaa wa Kiirani (pamoja na wale wa-Kiislamu) waliongeza makala zao na jitihada nyingine za kidijitali, kama vile "Google bomb" kulaani uvamizi wa Israeli katika ukanda wa Gaza, wanablogu wengine wanasema kwamba serikali ya Irani inatumia 'mwanya wa mgogoro wa Gaza' kukandamiza vyombo vya habari na jumuiya za kiraia ndani ya nchi hiyo.
Palestina: Mawasiliano na Gaza
Katika mazingira ya kawaida bila kiwango kikubwa cha wanaojua kusoma, usambaaji wa intaneti husimama kati ya asilimia 13 mpka asilimia 15 (Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa pamoja). Kutokana na mashambulizi yanayoendelea huko huko Gaza, uwezo wa kutumia intaneti umepungua sana. Japokuwa kuna idadi ndogo ya wanablogu wanaoandika moja kwa moja kutokea Gaza, wakazi wengine wengi wanatumia ujumbe wa maandishi wa simu za mkononi pamoja na simu nje ya nchi katika matumaini kwamba ushahidi wao utapata sehemu ya kuelezwa.
Palestina: Shule ya Umoja wa Mataifa Yashambuliwa na Makombora ya Israeli, Zaidi ya 40 wafariki
Takriban majira ya saa 12 za jioni (GMT +2), Idhaa ya Kiingereza ya Al Jazeera iliripoti kuwa shule moja ya Umoja wa Mataifa ilipigwa wakati makombora mawili ya vifaru yalipolipuka nje ya shule hiyo. Shule hiyo, iliyopo Jabaliya, ilianza kutumiwa kama makazi ya raia wa Gaza waliozikimbia nyumba zao au waliopoteza makazi yao. Zaidi ya watu 40 wameuawa. Jillian York anawasilisha maoni ya mwanzo kabisa katika ulimwengu wa blogu na twita.
Palestina: Gaza Haitafuti Aspirini Kwa Ajili Ya Kidonda Chake
Wapalestina wachache na wanaharakati wageni bado wanaweza kutuma ripoti za kile kinachoendelea kwenye ukanda wa Gaza kwa kutumia umeme wa jenereta pale inapobidi. Zifuatazo ni jumbe za blogu katika masaa 24 yaliyopita.