Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Februari, 2016
Mtumiaji wa Twita Nchini Saudi Arabia Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 10 na Viboko 2,000 kwa Kosa la “Kukufuru Dini”
Saudi Arabia imemhukumu mtumiaji wa mtandao wa Twita kifungo cha miaka 10 jela pamoja na viboko 2,000 kwa kosa la kuandika twi 600 "zinazoeneza imani ya ukana-Mungu" mtandaoni.
Polisi wa Kidini Thelathini Nchini Saudi Arabia Wahitimu Mafunzo ya Kukabiliana na Uchawi
Wajumbe thelathini wa Tume ya Kusimamia Maadili na Kukabiliana na Maovu wamemaliza mafunzo ya siku tano ya namna ya kukabiliana na uchawi, kuwatambua walozi na hata kuvunja laana zao.
Magazeti Nchini Iran Yabaini Udhalilishaji na Unyanyasaji wa Wanafunzi wa Afghanistan
“Hakuna matamko rasmi ya serikali yanayokemea uonevu dhidi ya wanafunzi wa Afghanistani. Tatizo ni mtazamo walionao wanajamii.”
Uandishi wa Habari ni Kosa la Jinai Nchini Bahrain
Mwandishi wa habari wa Marekani, Anna Therese Day pamoja na wenzake walishikiliwa nchini Bahrain, na kisha kurudishwa nchini mwao wakati wa kumbukumbu ya miaka mitano ya maandamano ya kuipinga serikali ya nchini Bahrain.