· Julai, 2012

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Julai, 2012

Basi la Watalii Raia wa Israeli Lashambuliwa Nchini Bulgaria

Watu wapatao saba wameuawa katika shambulio la la kijana wa Kiyahudi katika basi la kitalii lililokuwa katika uwanja wa ndege wa Burgus nchini Bulgaria. Ripoti zinadai shambulio linaonekana kuwa la kujitolea mhanga, lililofanywa na kijana alikuwa ama karibu na basi au alikuwa ndani ya basi.

31 Julai 2012

Palestina: Makala Kuhusu Kifo cha Arafat yaibua maswali

Kituo cha habari cha Al Jazeera hivi karibuni kilionyesha makala iliyohusu kifo cha utata cha rais wa Palestina Yasser Arafat kilichotokea mjini Paris mnamo Novemba, 2004. Makala hayo yanadai kwamba kiongozi huyo hakufa kifo cha kawaida, ila aliwekewa sumu ya poloni, madai ambayo yanaibua maswali mengi.

12 Julai 2012

Misri: Mubarak Afariki Dunia kwa Mara Nyingine

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak amewahi kufa angalau mara moja kwa kila baada ya majuma machache tangu kuanza kwa mapinduzi ya Misri, yaliyouangusha utawala wake uliodumu kwa miaka 32. Watumiaji wa mtandao wanaitikia tetesi za hivi karibuni kuhusu afya yake.

7 Julai 2012