Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Februari, 2009
Sudani: Maombolezo ya Mwandishi Maarufu wa Riwaya na Mahakama ya Kimataifa
Baada ya kimya kirefu, wanablogu wa Kisudani, wamerejea kwenye ulimwengu wa blogu kuongea, na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya hivi karibuni. Mawazo hayo yanayojumuishwa katika muhtasari huu ni pamoja na yale ya wanablogu tuliowazoea. Baada ya malalamiko kuhusu hali mbaya ya usalama wa afya kwenye Uwanja wa Ndege wa Khartoum, Msudani mwenye matumaini anaomboleza kifo cha mwandishi wa riwaya mashuhuri, Al- Tayeb Saleh.
Misri: Wanablogu Wafuatilia Milipuko ya Mabomu Mjini Kairo
Mtalii wa Kifaransa ameuwawa na watu wapatao 20 wamejeruhiwa wakati bomu lilipolipuka nje ya msikiti wa Al Hussein uliopo katika eneo la utalii la Khan Al Khalili mjini Kairo. Na wakati dunia ilipokuwa inaanza kufahamu ni kipi kilichokuwa kinatokea, wanablogu wa Misri waliingia kazini haraka, wakipashana habari za yanayotukia, taarifa, uchambuzi na hofu zao.
Bahrain: Mabloga Waungana Kupinga Uamuzi wa Kufungwa Kwa Tovuti
Wanablogu wa Bahrain wameujia juu uamuzi wa Waziri wa Habari wa nchi hiyo wa kuzuia upatikanaji wa tovuti mbalimbali, kadhalika kuzuia matumizi ya tovuti vivuli [proxy sites] zinazoruhusu watumiaji kuperuzi tovuti nyingine zilizozuiwa na zana za kuchuja habari. Ayesha Saldanha anaangalia maoni kutoka Bahrain.
Mashariki ya Kati: Vikwazo kama Silaha ya Kisiasa
Watu wengi wa Mashariki ya Kati wamesusia bidhaa za Israeli na Marekani kama jibu la mashambulizi ya Israeli huko Gaza. Tarek Amr anapitia yale wanablogu wanayosema kuhusu suala hili.