Mashariki ya Kati: Vikwazo kama Silaha ya Kisiasa

Watu wengi Mashariki ya Kati wamesusia bidhaa za Israeli na Marekani kama jibu la mashambulizi ya Israeli huko Gaza.

Bloga anayejiita Shirika la Habari la Kiarabu Lenye Hasira anaandika:

Katika nchi tano za Kiarabu kampeni mpya na nyeti iliyoratibiwa ili kususia bidhaa za Kimarekani imezinduliwa, na migahawa ya kahawa ya Starbucks ndio shabaha yake ya kwanza, ikifuatiwa kwenye orodha hiyo na maduka ya Nestlè, Coca-Cola, Johnson & Johnson pamoja na Burger King.

Miongoni mwa maduka yote yenye chapa ya Marekani, Starbucks ndio iliyokuwa inalengwa zaidi na kampeni hizo za kususia. Bloga Zeinobia wa Misri, anaandika:

Starbucks, tawi maarufu la Starbucks mjini Beirut lilifungwa kwa siku moja kufuatia maandamano ya kulipinga. Kuna wito umetolewa na kuitikiwa katika ulimwengu wa Waarabu kususia bidhaa za Marekani hasa 84268245 bidhaa ambazo zinazohusishwa na Israeli kwa njia moja au nyingine.

Halafu anaendelea:

Umma wa Waarabu unaamini kwamba Starbucks ya Marekani hulipatia Jeshi la Israeli, IDF mchango wa mwaka kutokana na ukweli kwamba mwanzilishi wa Starbucks ni Myahudi, na nikitaka kuwa mkweli, ukweli huo hautoshi kufikia hitimisho kwamba kampuni hiyo hutoa michango kwa jeshi la Israeli, lakini habari kama hizi zinaufanya umma wa Waarabu kufikiri mara mbili.
Uvumi wa Starbucks-Jeshi la Israeli ni uvumi wa siku nyingi hata kabla ya kufungua tawi lake nchini Misri, kampuni hiyo ilipingwa na ulimwengu wa Waarabu.
Nakumbuka siku moja nilipokea barua pepe inayohusu nembo ya Starbucks na historia yake, ikisema kwamba nembo hiyo ni alama ya binti mfalme wa Kiebrania aliyewakomboa Wayahudi waliokuwa Babeli wakati wa zamani ilhali hilo ni jambo jingine kabisa.

Kampeni hizo za kususia hazipo tu huko Uarabuni, kundi la wanablogu wa Kimarekani na Kipalestina KABOBfest linaripoti jinsi watu huko Malaysia wanavyoshiriki katika kampeni hizo:

Zaidi ya migahawa 2,000 inayomilikiwa na Waislamu nchini Malaysia imeondoa Coca-Cola kwenye orodha za vyakula katika jitihada za kuunga mkono migomo dhidi ya Israeli. Mashirika ya kizawa yanawashawishi wafanyakazi wa Coca-Cola, kadhalika na wale wa Starbucks na makampuni mengine, waziachee ajira zao.

Kutokea Jordan, Khobbeizeh pia anaandika kuhusu ususiaji wa Starbucks:

Howard Schultz ni Mzayonisti mwenye siasa kali zinzounga mkono jeshi la Israeli. Anawaunga mkono na mamia ya mamilioni kila mwaka kutoka katika kipato cha Starbucks, ni mmoja wa wadhamini wakubwa wa silaha.

Kwa hakika, bidhaa za Israeli zimegomewa na watu wengi, haya ndiyo alioandika bloga Body on the Line katika blogu yake:

Wakulima wanasema kwamba mazao yao mengi yamezuiliwa kwenye maghala kutokana na kusitishwa kwa ununuzi, na kuna hofu ya kupungua kwa uuzwaji wa matunda kuelekea nchi kama vile Jordan, Uingereza na nchi za Skandinavia.

Ilan Eshel, mkurugenzi wa shirika la wakulima wa matunda nchini Israeli, alisema kuwa nchi za Kiskandinavia pia zimekuwa zikisitisha uagizaji.

Bloga wa Kimarekani anayeishi Palestina, anaandika yale wasomi wa Uingereza wanayosema kuhusu mashambulizi ya Israeli huko Gaza:

Wasomi wa Uingereza wameandika barua ya wazi, iliyochapwa kwenye gazeti la Guardian, inayoitisha ususiaji, kuondoa vitega uchumi, na migomo:
“Ni lazima tufanye tunaloweza ili kuizua Israeli kushinda vita hivi. Israeli ni lazima ikubali kuwa usalama wake unategemea haki na kuishi salama pamoja na majirani zake, na siyo kwa kutegemea matumizi maovu ya nguvu.
“Tunaamini israeli lazima isitishe mara moja bila masharti mashambulizi yake huko gaza, isitishe ukaliaji wa mabavu kwenye Ukingo wa Magharibi, waache madai ya kumiliki au kuendesha himaya inayovuka mipaka yake ya 1967. Tuanitaka serikali ya Uingereza na watu wa Uingereza kuchukua hatua zote zinazowezekana za kuitaka Israeli ikubaliane na madai haya, kwa kuanza na programuya ususiaji, kuondoa vitega uchumi, na vikwazo.”
Mjini London wanafunzi pia walichukua hatua ya mshikamano na Gaza katika chuo cha Uchumi cha London:

Zaidi ya wanafunzi 40 waliendela na kampeni yao ya kukaa chini katika Chuo Cha Uchumi cha London leo hii ili kupinga machafuko huko Gaza.

Pia kuna asasi na tovuti ambazo zinalenga tu kusambaza habari juu ya kampeni kama hii, hii na hii.

Lakini kwa upande mwingine, wengine, kama vile bloga Crossroads Arabia hawakutilia mkazo sana kwenye kususia bidhaa:

Gazeti la Saudi liliripoti kwamba kususia bidhaa za Marekani ili kuwaunga mkono watu wa Gaza kumeanza kumea nchini Saudi Arabia. Kama ilivyowahi kutokea awali, ususiaji huu unaweza a) kupunguza hisia za kutokuwa na nguvu [za Waarabu] na b) kuumiza wamiliki wa Kiarabu pamoja na wafanyakazi wao, bila ya kuathiri uchumi wa Marekani, kinyume na vile anavyodai profesa wa Chuo Kikuu cha Abdulaziz.
Hata hivyo, ni wazi kwamba dhana ya kususa inaungwa mkono na wengi.

Kadhalika, bloga Jewlicious ameandika makala kumjibu Khobbeizeh:

Mimi si mshabiki wa Starbucks, au kahawa, lakini suala la Starbucks kuunga mkono Jeshi la Israeli kwa kiasi cha “mamia ya mamilioni kila mwaka” ni jambo ambalo ni vigumu kuaminika. Rafiki yangu Khobbeizeh, tukiweka pembeni ufundi wako wa kutumia Photoshop, wewe ni mbumbumbu.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.