Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Disemba, 2009
Podikasti: Mahojiano na Sudanese Drima
Sudanese Drima ni jina la bandia la mwandishi wa Kisudani wa Global Voices anayeishi nchini Malaysia. Katika mahojiano haya ya dakika kumi tunajadili jinsi uanahabari wa kijamii unavyoathiri Uislamu, mgogoro wa dafur, na masuala ya nafsi ya Uafrika-Uarabu katika Asia ya Kusini Mashariki.
Iran: Maandamano Tehran
Hii ni video inayoonyesha waandamanaji huko Manzarieh na Nyavaran mjini tehran wakiimba kauli mbiu dhidi ya utawala wa Kiislamu Jumamosi.
China na Iran: #CN4Iran
Jana, maelfu ya Wa-Irani waliingia mitaani ili kupinga dhidi ya utawala wa kiimla. Maandamano hayo yaliwakumbusha watu wa China juu ya vuguvugu la demokrasi la Tiananmen la 1989 na watumiaji...
Palestina/Gaza: Matayarisho ya Maandamano ya Uhuru Gaza
Ni kama wiki moja hivi mpaka Maandamano ya Uhuru Gaza yatakapoanza. Lengo lake ni kuonyesha mshikamano na Wapalestina na kuongeza ufahamu kuhusu vikwazo vinavyoizingira Gaza. Katharine Ganly anatazama baadhi ya matukio yaliyotokea katika maandalizi ya maandamano hayo.
Morocco: Mwanablogu Mwingine Atupwa Gerezani
Mnamo tarehe 14 Desemba, siku ya Jumatatu, mwanablogu Bashir Hazzam na mmiliki wa mgahawa wa Intaneti Abdullah Boukhou walihukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa huyo wa kwanza na mwaka mmoja kwa huyo wa pili pamoja na kulipa faini ya MAD 500 (sawa na dola za Marekani 63) kila mmoja katika mahakama ya Goulmim.
Misri: Makao Makuu ya Kuzimu Duniani
Wanablogu na wanaharakati wengi wa Kimisri wamekuwa wakikamatwa na Usalama wa Taifa katika nyakati tafauti kwa sababu mbalimbali –za kweli au za bandia –Wa7da Masreya aliwahoji wanablogu mbalimbali na kuweka makala ya kina kuhusu mbinu za utesaji na hila za kisaikolojia ambazo wanablogu wale wamekuwa wakikumbana nazo kwenye makao makuu ya Usalama wa Taifa katika wilaya ya Jiji la Nasr.
Israel: Kublogu Kwa Ajili Ya Mazingira Nchini Jordan
“Wanamazingira na Waandishi kutoka Palestina, Jordan na Israel watakutana huko Madaba, Jordan mwezi huu kwa ajili ya warsha ya siku 2: “Kublogu kwa Ajili ya Mazingira” tarehe 20-21 Desemba,” anaandika...
Tunisia: Mwanafunzi Atupwa Gerezani kwa Kuhojiwa na Chombo cha Habari
Wanaharakati nchini Tunisia wamezindua ukurasa wa Facebook na blogu ili kumuunga mkono Mohamed Soudani, 24, aliyetoweka mnamo tarehe 22 Oktoba 2009 nchini humo mara baada ya kufanya mahojiano na Redio Monte Carlo International na vilevile Redio France International. Tangia hapo marafiki walipata fununu kwamba alikamatwa na kutupwa korokoroni na kuteswa vibaya.
Iran: Maandano ya Siku ya Mwanafunzi kwenye YouTube
Maelfu ya waandamanaji hawakuujali utawala wa Kiislamu leo kwa kuandamana wakati wa siku ya mwanafunzi, wakiimba kaulimbiu dhidi ya Ali Khamenei, kiongozi wa Jamuhuri ya Kiislamu, na wakipinga sera ya mambo ya nje ya serikali.
Morocco: Kusherehekea Idi katika Sehemu za Mashambani
Wikiendi hii iliyopita, Wamoroko walisherehekea Eid Al-Adha. Wanablogu walioko sehemu za vijijini nchini Moroko wanasimulia simulizi zao kuhusu Eid ya mwaka huu. Kwa kuwa upatikanaji wa intaneti upo sehemu chache n amara nyingi ni wa aghali mno nje miji mikubwa, wengi wanaoblugu kutokea sehemu za mashamba ni Wafanyakazi wa Amani wa Kujitolea (PCVs) na kwa hiyo wako katika nafasi ya kuweza kutoa mitazamo kama wageni kutoka nje… walioko ndani.