Mnamo tarehe 14 Desemba, siku ya Jumatatu, mwanablogu Bashir Hazzam na mmiliki wa mgahawa wa Intaneti Abdullah Boukhou walihukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa huyo wa kwanza na mwaka mmoja kwa huyo wa pili pamoja na kulipa faini ya MAD 500 (sawa na dola za Marekani 63) kila mmoja katika mahakama ya Goulmim. Hazzam alifungwa kwa kosa la kile kinachoitwa “Kueneza habari za uongo zinazochafua sura ya ufalme kuhusu masuala ya haki za binadamu,” wakati kwa Boukhou pia ilikuwa kwa sababu hizohizo na pengine ilihusisha pia kutoa nafasi ya kusambaza taarifa hizo. Wanafunzi wengine watatu wamehukumiwa kwenda jela miezi sita na kulipa faini ya MAD 5000 (sawa na dola za Marekani 632) pamoja na Bashir na Abdullah kwa kuendesha mgomo haramu katika jiji la Taghjijt.
Bashir Hazzam ametuhumiwa kwa “Kueneza habari za uongo zinazochafua sura ya ufalme kuhusu masuala ya haki za binadamu,” baada ya kutiwa mbaroni mnamo tarehe 8 Desemba, iliripoti Kamati ya Kulinda Wanablogu, ikisema:
Mwanblogu wa Ki-Morocco, Bashir Hazem, alitiwa mbaroni mnamo tarehe 8 Desemba, 2009 kufuatia mgomo uliofanyika katika jiji la Tarjijt, ambapo wanafunzi walipambana vikali na vyombo vya usalama, na baada ya yeye kuwa amechapisha taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mapambano hayo katika blogu yake, na taarifa hiyo ilikuwa na saini za wanafunzi wanakamati waliotiwa mbaroni.
ANHRI, ambao ni Mtandao wa Kiarabu kuhusu Taarifa za Haki za Binadamu, ulilaani vikali kukamatwa huko kwa mwanablogu Bashir Hazzam. Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka (RSF) nao walilaani na kuhoji kwa nini hukumu ilitoka katika kipindi ambapo serikali ya Morocco inaanzisha programu ya kuhamasisha utumiaji wa Intaneti, ujenzi wa jamii iliyohabarika na uchumi wa dijitali:
Alors que le gouvernement marocain a présenté, en octobre dernier, un plan visant à améliorer l’accès à Internet afin de mieux intégrer le royaume à la société de l’information et à l’économie numérique, ces condamnations marquent un retour en arrière et montrent que la liberté d’expression sur Internet ne s’applique pas aux critiques des autorités. La multiplication d’arrestations de blogueurs ces deux dernières années nous inquiète profondément.
Kumekuwepo na maoni mengi yanayochapishwa katika Blogma baada ya tukio hili jipya la kufungwa kwa Mwanablogu. Mwanblogu Larbi [RF] alichapisha tamko la RSF akiongeza:
Voici donc où nous en sommes : dans un pays qui jette en prison des citoyens pour le seul crime d’avoir exercé pacifiquement leur droit à la liberté d’expression, à la manifestation … Un drôle de pays qui, aussitôt la page des années de plomb tournée, en a ouvert une autre avec son lot d’exactions, de condamnations arbitraires, de violences policières et d’atteinte aux droits humains.
Mwanablogu na mwanaharakati wa haki za binadamu, Samira Kinani, aliripoti kuhusu maandamano ya kuwaunga mkono akina Bashir Hazzam na wengine wale waliotiwa ndani kwa maoni yao mbele ya Bunge la Morocco katika jiji la Rabat mnamo tarehe 15 Desemba. Maandamano hayo yalivunjwa kwa nguvu na polisi. Ibn Kafka [fr], mwanablogu na mwanasheria, alichapisha picha kutoka katika blogu ya Samira na kuandika maoni haya:
… les compagnies mobiles d’intervention (CMI) tabassent de paisibles femmes quadra- ou quinquagénaires, sans aucune gêne – imaginez ce que ça peut être avec de jeunes hommes à Taghjijt.
Wanablogu wengine wanazidi kuwaunga mkono Bashir Hazzam. Kacem El-Ghazali [Ar] ambaye anaandika blogu yake katika bahmut, anaandika akisema:
نتضامن مع المدون البشير حزام ورفاقه…. مستنكرين ما طالهم من اعتقال تعسفي تحكمي ومطالبين باطلاق سراحهم والاستجابة لمطالبهم… في مغرب العهد الجديد، عهد الحريات والديموقراطية، مغرب الخطابات الرسمية التي ما تلبث أن يماط اللثام عن حقيقتها، لتبقى مجرد تهافت يتهافته كل من له مصلحة في ذلك، ومنفعة في استمرار واقع الظلم والاستبداد والتدجين
Kampeni ya kusaidia kuwatoa gerezani mwanablogu Bashir na wenzake imezinduliwa. Ukurasa wa Facebook [Ar] ulianzishwa ili kuwasaidia Bashir Hazzam, vilevile kuna tovuti imeanzishwa na inayoitwa Free Bashir, vilevile kuna akaunti ya Twita. Kampeni ya picha ya Flickr nayo imeanzishwa; picha hizo zinaweza kutumwa kupitia ukurasa wa Facebook au kwa anwani hii ya baruapepe freebashirhazzem@gmail.com.
Katika makala ya hivi karibuni, Naoufel [Ar] anajiuliza kama kuanza kuandika kwenye blogu ndiyo hatua ya kwanza ya kuelekea gerezani:
لابد أنك -في يوم ما- سألت عن التدوين.. و كيف تصبح مدونا.. و لا بد أنك وجدت عشرات الأجوبة المختلفة.. الغبية منها و المقنعة ..أمنحك الان جوابا غبيا اخر : التدوين هو أول خطوة الى السجن
Natumaini kwamba jambo hili halitatukia kamwe nchini Morocco.