Morocco Yaondoa Vikwazo Dhidi ya Vitumizi vya VoIP Kuelekea Kongamano la Tabia Nchi la Umoja wa Mataifa.

An old phone at a hotel in the city of Tangier. Photo by Steve Calcott

Simu ya zamani katika hoteli moja iliyopo katika jiji la Tangier. Picha na Steve Calcott.

Serikali ya Morocco katika hali ambayo haikutarajiwa imeviacbhia huru vitumizi vya VoIP ambavyo hapo awali iliondoa matumizi ya mawasiliano ya sauti ya vitumizi kama vile WhatsApp na Skype tangu Januari 2016. Tangu Oktoba 24, watumiaji wa mtandao wa intaneti wa nchini Morocco wameweza kutumia vitumizi hivi pamoja na vingine bila ya kutumia VPNs au vitumizi vingine vinavyoficha utambulisho wa mtuaji wa mtandao wa intaneti.

Mamlaka ya Usimamizi wa tasnia ya Mawasiliano ya nchini Morocco, Wakala wa Usimamizi wa Mawasiliano (inayofahamika kwa ufupisho wa maneno ya Kifaransa kama ANRT), hadi sasa haijatoa tamko lolote rasmi ikiwa kuondolewa kwa makatazo haya ni ya muda tu au ni matokeo ya kubadilika kwa sera. Hata hivyo, watumiaji wa mtandao wa intaneti wanaona kuwa katazo hili limendolewa kutokana na Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabia NChi (COP22) unategemewa kufanyika katika jiji la Marrakesh kati ya NOvemba 7 na 18. Wanatarajia kuwa, katazo litaendelea hat mara tu baada ya kumalizika kwa kongamano.

Huduma za VoIP zinapatika Morocco kwa sasa kwa sababu ya #COP22. Vinginevyo, sisi kama Raia wa Morocco, tunashindwa kuzitumia kwa takraibani mwaka mzima. Aibu yenu ANRT

Huduma za VoIP zimewezeshwa nchini Morocco. Wageni 30,000 ni bora kuliko raia wa Morocco wapatao milioni 30.

Ili kukwepa kuonekana kama ni nchi ya mabavu wakati wa kongamano la tabia nchi #COP22, nchi ya Morocco imerejesha kwa muda huduma za VoIP

Mapema mwaka huu, Mamlaka ya Uthibiti wa Mawasiliano iliweka katazo la kutumia vitumizi vyenye matumizi ya VoIP ikiwemo ya WhatsApp, Skype na Viber chini ya sheria ya nchi ya Mawasiliano na Posta ya mwaka 1996 iliyoanzisha utaratibu wa uhalali wa kutoa huduma za simu za sauti.

Pamoja na maandamano yaliyowakutanisha watumiaji wa mitandao waliojawa na ghadhabu, walianzisha maandamano ya kuzisusia kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano, huduma hazi hazikuwahi kurudishwa. Suala la Morocco si ngeni. Mataifa mengine kadhaa ya katika ukanda wa MENA kwa uchache au moja kwa moja kwa uchache zinafunga angalao kitumizi kimoja cha huduma ya sauti ya simu kama jinsi ramani hapa iliyoandaliwa na from angry users who launched a two-day boycott against telecom operators, access to these services have not been reinstated. The case of Morocco is not unique. Several other governments across the MENA region partially or fully block at least one VoIP application, as the map below by igmena.org inavyoonesha.

Bans on VoIP services across the Middle East and North Africa region. Map by igmena.org

Kuzuiwa kwa VoIP maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati na Eneo la Africa Kaskazini. Ramani na igmena.org

Katika kutafiti suala hili, Mpango wa Utafiti wa Ufuatiliaji wa InternetI iGMENA yaandika kuwa kufungia vitumizi vya VoIP mara nyingi kunahamishishwa na kutaka “kulinda maslahi ya wamiliki wa mitandao ya simu, ambapo mengi ya makampuni yanayohodhi yakiwa kwa kiasi fulani yanamilikiwa na serikali.”

Hata hivyo, makatazo haya yanaambatana na mtikisiko wa uchumi. Kwa mujibu wa taarifa ya Kituo cha Maendeleo ya Teknolojia cha Brookings ya gharama za kuzuia mtandao wa intaneti pamoja na usumbufu, hatua ya Morocco ya kuzuia vitumizi vya VoIP imeligharimu Taifa kiasi cha Dola za Marekani milioni 320 katika muda wa siku 182. Kufuatia katazo la mwezi Januari, wajasiriamali wa nchini Morocco pia walibainisha kuwa kuzia utoaji wa huduma za intaneti kungeweza kukwamisha maendeleo ya biashara change, hususani zile zinazotegemea huduma za vitumizi vya VoIP kwa ajili ya kuwasiliana na wateja wao wa kimataifa.

Pamoja na kuathiriwa kwa biashara, kuzuia vitumizi vya upigaji simu na kupokea au kutuma jumbe wakati mwingine ni suala la patapotea, husuani kwa nyakati za hali tete na machafuko. Mapema mwezi huu nchini Yemen, wanamgambo wa Houthi waliripotiwa kuzuia WhatsApp, kuweka vikwazo kiasi cha raia kushindwa kuwasiliana, kutoa taarifa za usalama wao na kuasambaza taarifa katika nchi ambayo makumi mawili ya tovuti za habari zimefungwa tangu kuanza kwa machafuko.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.