Iran: Maandano ya Siku ya Mwanafunzi kwenye YouTube

Maelfu ya waandamanaji hawakuujali utawala wa Kiislamu leo kwa kuandamana wakati wa siku ya mwanafunzi, wakiimba kaulimbiu dhidi ya Ali Khamenei, kiongozi wa Jamuhuri ya Kiislamu, na wakipinga sera ya mambo ya nje ya serikali. Vilevile walichoma picha za watawala wa Kiirani. Kwa mujibu wa tovuti kadhaa za habari, vikosi vya ulinzi vilipambana na wanafunzi na kuwatia nguvuni baadhi yao. Kama kawaida, wananchi wa Kiirani walizungumzia tukio hili la leo wakitaka dunia ijifunze kuhusu tukio hilo.

“Nini kimetokea kwenye fedha za mafuta”

Kwenye Chuo Kikuu cha Tehran, waandamanaji waliimba kwa sauti “Kuanguka kwa dikteta” na “Nini kimetokea kwenye fedha za mafuta? Zimeingia kwenye mifuko ya Basijis (Wanajeshi wa Kiislamu).”

“Vikosi vya Kijeshi ungeni mkono”

Katika chuo kikuu cha Amir Kabir University, pia kikiwa Tehran, wanafunzi walipiga kelele kama: “Apigwe chini dikteta,” “Majeshi ungeni mkono,” na “Msiogope”.

Chini na Khamenei katika mitaa ya Tehran


Kumbukeni Mashahidi

Chuo Kikuu cha Elmo Sanat mjini Tehran waliandamana wakiwa na picha ya Kianoush Asa, mwanafunzi aliyeuawa na vikosi vya ulinzi majira ya kiangazi mwaka 2009.

Waandamanaji waliandamana katika miji mingineyo kama Mashad

…na Kerman ambapo walipiga kelele “beki mlinda mlango mchukue Mahmoud [Ahmadinejad, rais wa Iran]”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.