Habari kutoka 15 Disemba 2009
Barbados, Trinidad & Tobago:Plastiki na Uchafuzi wa Mazingira
“Fanya matembezi kwenye pwani yoyote nchini Barbados – na utaona uchafu wa plastiki uliosukumwa ufukweni”: Barbados Free Press anauliza kama uuzaji wa chupa za plastiki za maji uwekewe vikwazo, wakati...
Tunisia: Mwanafunzi Atupwa Gerezani kwa Kuhojiwa na Chombo cha Habari
Wanaharakati nchini Tunisia wamezindua ukurasa wa Facebook na blogu ili kumuunga mkono Mohamed Soudani, 24, aliyetoweka mnamo tarehe 22 Oktoba 2009 nchini humo mara baada ya kufanya mahojiano na Redio Monte Carlo International na vilevile Redio France International. Tangia hapo marafiki walipata fununu kwamba alikamatwa na kutupwa korokoroni na kuteswa vibaya.
Iran: Maandano ya Siku ya Mwanafunzi kwenye YouTube
Maelfu ya waandamanaji hawakuujali utawala wa Kiislamu leo kwa kuandamana wakati wa siku ya mwanafunzi, wakiimba kaulimbiu dhidi ya Ali Khamenei, kiongozi wa Jamuhuri ya Kiislamu, na wakipinga sera ya mambo ya nje ya serikali.