Morocco: Kusherehekea Idi katika Sehemu za Mashambani

Wikiendi hii iliyopita, Wamoroko walisherehekea Eid Al-Adha, au Sherehe ya kutoa kafara, ambayo mara nyingine inajulikana nchini Moroko kama Eid Al-Kabir, au “sherehe kubwa,“ tofauti na Eid al-Fitr, inayojulikana kwa lugha ya mtaani kama Eid al-Sghir, au “Sherehe ndogo.” Wakati siku kuu zina maana inayofanana na utamaduni uleule katika nchi zote za kiislamu, maadhimisho yenyewe mara nyingi huwa ni ya aina ya tofauti kwa kila sehemu.

Erin anaeleza juu ya kondoo wa familia: “hakuwa na wazo la nini kinachomjia.”

Erin anaeleza juu ya kondoo wa familia: “hakuwa na wazo la nini kinachomjia.”


Wanablogu walioko sehemu za vijijini nchini Moroko (ambazo hujulikana kama bled) wanasimulia simulizi zao kuhusu Eid ya mwaka huu. Kwa kuwa upatikanaji wa intaneti upo sehemu chache n amara nyingi ni wa aghali mno nje miji mikubwa, wengi wanaoblugu kutokea sehemu za mashamba ni Wafanyakazi wa Amani wa Kujitolea (PCVs) na kwa hiyo wako katika nafasi ya kuweza kutoa mitazamo kama wageni kutoka nje… walioko ndani.

Erin, mfanyakazi wa kujitolea anayeblogu katika Reflections and Experiences in Al Maghreb Al Aqsa, anaelezea tamaduni za Eid za familia yake ya kufikia, anasema:

Jumamosi asubuhi, familia yangu ya kufikia ilichinja kondoo mmoja na mbuzi wawili kwa jili ya sherehe za Idi. Hii inafanyika kwa kumkumbuka Abraham, ambaye alikuwa tayari kumtoa mwanae wa pekee kafara kwa Mungu, kabla Mungu hajamwambia kumtoa kondoo badala yake. Ingawa familia za Kiislamu duniani kote zinafanya kitendo hiki, watu husherekea kwa namna tofauti. Familia nyingine hutoa nyama yote kwa wale wenye uhitaji, wakati wengine (kama famialia yangu ya kufikia) hula mpaka kiungo cha mwisho, na hubaki na nyama itakayowatosha kwa miezi miwili au zaidi.

Joy in Morocco aliweka picha hii katika blogu yake

Joy in Morocco aliweka picha hii katika blogu yake


Joy in Morocco, ambaye pia ni mfanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps, anaandika juu ya kitu anachokishukuru nchini Morocco, na vilevile kaweka picha ya mwanamke kutoka kijijini kwake anayepika wakati wa Eid:

Joy in Morocco aliweka picha hii kwenye blogu yake

Ukaribu wa Wamoroko na masuala ya chakula. Nyama ya kondoo huwa haiji kwa mapakacha yaliyogandishwa. Wanachinja. Wanaandaa nyama yote na kuanza kuibanika. Vivyo hivyo ni kuhusu uhusiano wao na matunda na mboga mboga, hasa katika mkoa wangu. Kila kitu huja kutoka kwenye mashamba yao, kwa jinsi ilivyo.

Mfanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps anayeblogu kwenye oclynn in morocco hakuwa shabiki wa siku kuu. Mwanablogu huyo anaeleza:

Moshi unaotokea kwenye vichanja vya kubanikia ukipanda kutoka kwenye mapaa ya varanda za nyumba wakati vichwa na makongoro ya miguu ya kondoo yakienda kwanza kwenye moto. Nikisikiliza kelele za kondoo wa jirani yangu kupitia paa letu wakati akifa (na kwa nini inaonekana kuchukua muda mrefu?). Kondoo walichinjiwa kwenye paa, mlango wa pili na upenuni mbele ya nyumba. Kila mahali. Damu ikitiririkia kwenye mifereji ya maji. Ni lazima iwe L’eid Kbir. Siyo siku kuu niipendayo, lakini ni takatifu kuliko zote kwenye dunia ya Kiislamu.

Kupulizia mapafu ya kondoo wa Idi.

Kupulizia mapafu ya kondoo wa Idi.


Bado mfanyakazi mwingine wa kujitolea wa Peace Corps ambaye blogu yake inaitwa From the Cold Land with the Hot Sun anatupa uzoefu wake unaofurahisha kutokana na siku kuu, kwa kutumia picha:

Ingawa ningependa kubadilisha uelekeo kutoka kwenye upande unaokerehesha na kuburudisha wa sherehe kwa ajili ya upande ule unaofaa kimaadili na unaochosha, nilishuhudia wasaa wa kuangusha taya wakati wa kumchuna mnyama tendo ambalo siwezi kujizuia kuliandika hapa. Wakati wa kuondoa mapafu kutoka kwenye kifua cha kondoo aliyening’inizwa kichwa chini miguu juu, jamaa mtaratibu aliyekuwa amechafuka damu akiwa ameyashikilia kwa sehemu ya koromeo iliyokuwa imebaki kiasi cha kuonekana na wote. Halafu akapuliza kwa nguvu kupitia tundu la koromeo hilo, akisababisha mapafu yajae upepo –yenye rangi nyekundu isiyokoza, yaking’aa, na ya ajabu kwa jua la asubuhi. Ilikuwa poa sana.

Cynthia, mwanablogu wa The Couscous Chronicles, ni mfanyakazi mwingine wa Peace Corps anayeandika kuhusu siku kuu. Anaeleza kwa nini inakuwa vizuri sana kuwa na ‘familia’ nchini Moroko:

Mwaka huu ulikuwa ulimwengu mzuri zaidi kuliko mwaka jana kwa sababu tu nilichagua kusherekea na majirani zangu (ambao kwa kweli wamekuwa familia yangu hapa) na familia yao kubwa, ambayo ni ya watu wenye bashasha na wa ajabu sana. Mwaka uliopita nilijisikia kama vile napelekwa kutoka nyumba hadi nyumba, nikinywa chai na kula nyama na nikisikia vibaya muda wote, lakini mwaka huu nilijisikia kama sehemu ya sherehe. Kujisikia kama sehemu kabisa ya familia kunafanya sherehe ziwe jambo la kusisismua sana.

Mwisho lakini sio kwa umuhimu, Reading Morocco anatupa mfulululizo wa onyesho la picha kutoka kwenye kijiji chake Kusini mwa Moroko, zikihusishwa na Leila Alaoui:

Eid Al Adha from aida alami on Vimeo.

Eid Al Adha kutoka aida alami kwenye Vimeo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.