· Mei, 2009

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Mei, 2009

Tajiri Wa Kimisri Ahukumiwa Kifo

  27 Mei 2009

Wamisri walishuhudia hukumu isiyotarajiwa katika historia ya vyombo vya sheria nchini humo: Bilionea Hesham Talaat Moustafa, pamoja na mamluki wake (mpiga risasi wa kukodi) Mohsen El Sokari wamehukumiwa adhabu ya kifo kutokana na kuhusika kwao katika mauaji ya mwimbaji wa Kilebanoni Suzanne Tameem. Mauaji hayo ya kinyama yalitokea huko Dubai, UAE, na hukumu iliyotolewa Alhamisi imesababisha mshtuko na mshangao wakati wanablogu walipojaribu kukubaliana na yaliyotukia.