· Februari, 2011

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Februari, 2011

Misri: Picha Zinapoongea Zaidi Ya Maneno

  4 Februari 2011

Kadri ya watu milioni tayari wapo kwenye viwanja vya (Ukombozi) vya Tahrir jijini Cairo wakiimba, na kumtaka Mubarak aondoke. Maandamano ya kumpinga Mubarak yamekuwa yakifanywa nchini misri kwa siku 11 mfululizo na siku ya leo imepewa jina la Ijumaa ya Kuondoka au Ijumaa ya Mwisho. Hapa kuna baadhi ya picha zilizotumwa kwa njia ya Twita na watu waliopo kwenye eneo hilo, zinazoonyesha umma unaoandamana kuelekea kwenye viwanja (vya Tahrir), wanavyopekuliwa kwa makini katika vituo vya ukaguzi vilivyowekwa ili kuwalinda waandamanaji wa amani mbali na wahuni waliolipwa na serikali.

Misri: El Baradei – Rafiki au Adui wa Waandamanaji?

  2 Februari 2011

Kiongozi wa upinzani nchini Misri Dr Mohamed El Baradei alifanya ziara fupi kwa maelfu ya waandamanaji wanaompinga Mubarak, walioweka kambi kwenye viwanja vya Tahrir jijini Cairo, dakika chache zilizopita. Maoni kutoka Twita yanafuata.