Misri: El Baradei – Rafiki au Adui wa Waandamanaji?

makala hii ni sehemu ya ukurasa wetu maalum wa Maandamano ya Upinzani Misri 2011.

Kiongozi wa upinzani nchini Misri Dr Mohamed El Baradei alifanya ziara fupi kwa maelfu ya waandamanaji wanaompinga Mubarak, walioweka kambi kwenye viwanja vya Tahrir jijini Cairo, dakika chache zilizopita.

Ufuatao ni mvumo ambao ziara hiyo imeuanzisha:

@Mme_Bavarde RT @sharifkouddous:Baradei ambaye anaonekana kuwa hajapotoka, anaheshimika. Lakini aliishi mbali kwa muda mrefu sana, hakuungana na maandamano ya awali & na mapinduzi haya yaliandaliwa bila ya msaada wake

@sharifkouddous Watu wanagawana mikate. Wanaketi na kuimba. Wanamsubiri Baradei. #Egypt

@mikeedwards606 RT @parvezsharma: KWELI KABISA! @gharbeia Tahrir sq #Baradei hawahutubii watu bali waandishi wa habari wakati watu wanaswali huku wakielekea upande tofauti #Jan25

@tameryaza jinamizi la #Mubarak, Mohamad El-Baradei amejiunga na waandamanaji jioni hii kwenye “Viwanja vya Ukombozi”… #egypt #tunisia #turkey #usa

@sultanalqassemi: El Baradei awasili Meydan Tahrir. Ukurasa wa Al Arabiya http://yfrog.com/h81yiyj http://yfrog.com/gznmqtzj

@Dima_Khatib Al Baradei anaripotiwa kuwa yuko tayari kuondoka kwenye viwanja vya Tahrir, au pengine ameshaondoka… nia yake ni? Matembezi ya kindugu? #egypt #cairo #jan25

@whisper1111 RT @jeremyscahill: Aah RT @sharifkouddous Watu wanasema baradei alizimia sijui halafu akaenda nyumbani. Watu wanasimama na kuondoka huku wamevunjika moyo. #Egypt

@FromJoanne RT @parvezsharma: Kabla sijaenda mapumziko. Hebu fikiria hili tafadhali. #Baradei kila wakati huwa anataka kuongea na waandishi wa habari wa ki-Magharibi na sio kuongea na wananchi #Egypt #Jan25

@Nashmiyya RT @lo2lu2a: #Baradei waandamanaji wa upinzani 2: “Tumo kwenye zama mpya” “Kile tulichoanzisha hakiwezi kugeuzwa nyuma”. Je anayateka (maandamano) & na kujiteua kama kiongozi? #egypt

@ShugsssRT @IAmTheStarchild: @shugsss Baradei ni chale anayejaribu kuyateka mapinduzi. Hicho ndicho kinahitajika kuwekwa wazi ;)

@NooRSR RT @mzaher: haya, El Baradei ana akaunti rasmi ya Twita @elbaradei. #justsaying #Egypt #Jan25

@SocialistViews Historia ya El-Baradei ni ya mtu mwenye siasa za wastani ambaye amekuwa akipinga mfarakanao wa moja kwa moja na utawala wa #Mubarak regime http://socwrk.org/9333 #p2 #jan25

@EvilLolly: haya ni maoni yang utu lol, lakini nina mashaka kuhusu Baradei Swali ambalo kila mmoja anapaswa kuuliza ni amefanya nini kustahili kuongoza?!

@0ssarian42 RT @syrianews: Baradei ni zawadi kwa Mubarak – unautenganisha upinzani RT @Sandmonkey: Niliondoka kwenye maandamano muda mfupi baada ya baradei kujiunga, maelfu bado wako pale

@ruwaisreviews RT @EhabZ: Mara Firauni anapoanguka, Baradei anapaswa atumikie kama kiongozi wa mpito, na kuruhusu uchaguzi muda mfupi katika mfupi ujao.

@oasanchez RT @democracynow: RT @sharifkouddous: Baadhi wanataka Baradei awemo katika namna fulani ya serikali ya mpito. Hisia zimechanganyika.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.