Makala hii ni sehemu ya ukurasa wetu maalum wa Maandamano ya Upinzani Nchini Misri 2011.
Kadri ya watu milioni tayari wapo kwenye viwanja vya (Ukombozi) vya Tahrir jijini Cairo wakiimba, na kumtaka Mubarak aondoke. Maandamano ya kumpinga Mubarak yamekuwa yakifanywa nchini Misri kwa siku 11 mfululizo na siku ya leo imepewa jina la Ijumaa ya Kuondoka au Ijumaa ya Mwisho.
Hapa kuna baadhi ya picha zilizotumwa kwa njia ya Twita na watu waliopo kwenye eneo hilo, zinazoonyesha umma unaoandamana kuelekea kwenye viwanja (vya Tahrir), wanavyopekuliwa kwa makini katika vituo vya ukaguzi vilivyowekwa ili kuwalinda waandamanaji wa amani mbali na wahuni waliolipwa na serikali:
@monasosh: Mapinduzi ya Misri Kiboko! #Jan25 :) http://yfrog.com/h7tl5bj
@beleidy: Kwenye kituo cha ukaguzi cha daraja la At qasr El nil #jan25 egypt http://twitpic.com/3wckhq
@monasosh: Idadi ya ajabu na msururu mrefu wa watu wanaosubiri kuingia kutokea daraja la kasr el nile #Jan25 http://yfrog.com/h0efpmmj
@ElFoulio: Tayari keshapata ujumbe, uko wazi kabisa #Tahrir #Jan25 http://twitpic.com/3wcjp2
@nohaHMsafar: Moja ya mabango ya waandamanaji, nimelipenda sana! 7asbi allah 3alek ya Mubarak! #egypt #jan25 http://yfrog.com/gz25tlqj
@norashalaby: Mistari mirefu ili kuingia tahrir #Jan25 http://yfrog.com/gyuhzqwj
@mideastmedia: PICHA: Mchoro uliopo Viwanja vya Tahrir uliochorwa baada ya hofu kugubika matangazo ya Televisheni ambayo yanaelezea hali ilivyo nchini Misri, au itakavyoharibika http://yfrog.com/gzjq7anj #jan25
@Gsquare86: Lango la Kasr El Nile lilikuwa na mpangilio mzuri sana na usalama wa hali ya juu http://yfrog.com/h4enlpxj
Makala hii ni sehemu ya ukurasa wetu maalum wa Maandamano ya Upinzani Nchini Misri 2011.