Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Oktoba, 2009
Palestina: IDF Yachoma Moto Magari Ya Wapalestina
Kwenye Do Unto Others, Samuel Nichols anaandika kuwa doria ya jeshi la Israel imeanza kuchoma moto magari ambayo yanakamatwa yakijaribu kuvuka mpaka kutoka Ukanda wa Magharibikuingia Israel. Ametundika video hapa.
Uchaguzi Tunisia: haki Bila Ya Upendeleo!!?
Rais wa Tunisia Zine Al Abidine Ben Ali ameshinda uchaguzi kwa kipindi cha tano kwa asilimia 89.62 ya kura zote. Chama chake cha Democratic Constitutional Rally kilishinda viti vya bunge 161 katika viti 214. Wanablogu wa Tunisia wanatoa maoni katika makala hii.
Misri: Watawala Wa Kiimla na Wake Zao
Baada ya kuziangalia picha za mke wa Rais wa Cameroon, Mmisri Zeinobia anasema: “Sijui ni ni kiasi gani cha pesa alichotumia kwa ajili ya nywele zake na muonekano wake lakini...
Syria: Mwanaharakati wa Haki Za Binaadamu Mwenye Umri wa Miaka 80 Akamatwa
Omar Mushawah ameripoti [ar] kukamatwa kwa Haytham al-Maleh, mwanasheria wa Ki-Syria na mtetezi wa haki za binaadamu ambaye pia alitumia muda wa miaka 6 jela kati ya 1980 na 1986...
Uanaharakati na Umama Barani Asia
Je, mwanamke anatoa sadaka zipi ili kupigania jambo analiamini? Je, watoto wake wanaathiriwa vipi na mateso yanayoelekezwa kwake? Makala hii inachambua kwa kifupi maisha ya wanawake wanaharakati katika Asia ambao pia ni ma-mama.