Omar Mushawah ameripoti [ar] kukamatwa kwa Haytham al-Maleh, mwanasheria wa Ki-Syria na mtetezi wa haki za binaadamu ambaye pia alitumia muda wa miaka 6 jela kati ya 1980 na 1986 kwa kudai mabadiliko ya kikatiba. Al-Maleh pia ni mwanzilishi mwenza wa Jumuiya ya Haki za Binaadamu ya Syria.