25 Oktoba 2009

Habari kutoka 25 Oktoba 2009

Bhutan: Mpito Usio na Mikwaruzo Kuelekea Demokrasi

  25 Oktoba 2009

Tshering Tobgay, kiongozi wa chama cha upinzani katika Bunge la Taifa la Bhutan, anatoa maoni kuwa: “mpito wetu kuelekea demokrasi, kwa hakika, umetukia bila mikwaruzo. Umetukia bila mikwaruzo kiasi kwamba wengi wetu walikuwa hata hawaufuatilii.”

Marekani: Wanandoa wa rangi tofauti wanyimwa cheti cha ndoa

  25 Oktoba 2009

Juma lililopita huko Hammond, Louisiana, wapenzi wawili walituma maombi ya kibali cha kufunga ndoa na walikataliwa kwa misingi ya rangi zao tofauti. Afisa wa kutathmini na kuandikisha nyaraka (Muamuzi wa Amani) alidai kuwa “ndoa baina ya watu wa rangi hazidumu” na alisema kuwa anafanya hivyo “kwa ajili ya watoto.”