Uchaguzi Tunisia: haki Bila Ya Upendeleo!!?

Kama ilivyotabiriwa, rais Zine Al Abidine Ben Ali ameshinda uchaguzi kwa mara ya tano. Ambalo halikutarajiwa ni kuwa angeshinda kwa asilimia 89.62 ya kura zote. Utabiri ulikuwa kwamba angepata kura zaidi.

Chama kinachotawala cha Ben Ali, Democratic Constitutional Rally nacho pia kilifanya vizuri. Kilishinda viti vya bunge 161 katika viti 214. Viti 53 vilivyobaki vilinyakuliwa na vyama sita tofauti: Movement for Democratic Socialists, viti 16; Party of People's Unity, kinachoongozwa na Mohamed Bouchiha, viti 12; chama cha Union of Democratic Unionists cha Ahmed Inoubli, viti 9; Social Liberal Party, viti 8; Party of Greens for Progress, viti 6 na chama cha Ettajdid cha and Ahmed Brahim, viti 2.

Chama tawala kilitangaza haki na usawa katika uchaguzi wa 2009. Lakini viongozi wa upinzani na wanablogu wana maoni mengine: wanafikiri kuwa vitendo vya ukandamizaji na udhibiti mkali kwenye taratibu za uchaguzi vilitawala uchaguzi wa rais na wabunge nchini Tunisia mnamo tarehe 25, Oktoba 2009.

Arabasta anasema kwa kejeli:

مبروك عليكم ما عملتو
نتوجه بالشكر أولا إلى الشعب التونسي اللي قام بواجبو الإنتخابي في كنف الديموقراطية و الشفافية و الروح الرياضية البارح و إنتخب رئيس جديد للبلاد و مجلس نواب أخر لمدة خمسة سنين. الإختيار هذا كان محكم و مدروس و حتى واحد ما حاول يأثر على العباد و حتى من التلفزة و الصحافة كانو في المستوى و عطاو وقت متساوي لكل المترشحين و الأنصار متاعهم بقطع النظر عن
قربهم أو بعدهم عن السلطة
نتوجه بالشكر زادة لسيادة رئيس الجمهورية (لمدة 5 سنوات أخرى) و نعتذر عن عدم الدعوة و التصويت ليه و نستنكر و نشجب
التصرفات المشينة هذي أما نذكر أنو عمري ما شككت في نزاهة الإنتخابات و حريتها، فمن المعروف أنو في حالة تزوير الإنتخابات النتائج تكون من نوع 99،98% لكن الملاحظ النزيه يعرف أنو نتيجة 2009 ما تبعدش برشة على النسبة اللي ربح بيها شيراك في 2002 في فرنسا و لذا فالإنتخابات هذي إرتقت بينا إلى مصاف الدول العظمى و المتقدمة

Hongera kwa ulichofanya!
Shukrani nyingi ziwafikie kwanza raia wa Tunisia ambao walitimiza wajibu wao jana katika uchaguzi ndani ya muundo wa demokrasia na usawa. Walimchagua rais mpya wa nchi na bunge jipya kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Chaguo lilikuwa la busara na lililotafakariwa vyema. Hakuna aliyejaribu kuwashawishi watu na hata idhaa za televisheni na vyombo vya habari vya maandishi havikufungamana na upande wowote na vilihakikisha kuwa wagombea na wafuasi wao wanapata nafasi sawa bila kujali uhusiano wao na serikali.
Shukrani zangu pia zimfikie rais (kwa miaka mingine mitano) na naomba radhi kwa kutomuunga mkono na kutokumpigia kura. Ninailaani tabia hii ya aibu japokuwa ninakumbuka ukweli kuwa sijawahi kutilia shaka kutofungamana kwenu na upande wowote wakati wa uchaguzi. Kama inavyoeleweka kuwa kama pangetokea udanganyifu basi matokeo yangekuwa asilimia 98.99. Lakini msimamizi asiyefungamana na upande wowote anafahamu kwamba matokeo ya 2009 hayana tofauti sana na yale ya 2002 nchini Ufaransa wakati Chirac aliposhinda uchaguzi. Na hiyo ndio sababu inayotufanya tuweze kusema kuwa uchaguzi huu umetupandisha na kufikia daraja la nchi zilizoendelea na mataifa makubwa.

Nakhlet Wed El Bey (Mtende wa mto Bey) anaandika katika lugha ya Kitunisia:

أنا لا أشكك في نزاهة التمثيلية الإنتخابية

آش كان عليه لو كان حلّينا اللعب شويّة
و نزعنا الأكمام من أفوه المعارضة الحقيقية
لإنتصر الرئيس بسبعة و سبعين في المية
و انتزعنا من قلوب الرعايا النفاق و السكيزوفرينية

Sihoji haki na kutopendelea kwenye maigizo ya uchaguzi wa Tunisia.
Je ingekuwaje kama tungelikuwa na uwezo zaidi
Na kuondoa viziba midomo kutoka kwenye mdomo wa upinzani wa kweli
Hapo rais angelishinda kwa asilimia 77.7
Na tungeondoa unafiki na wehu kutoka kwenye mioyo ya watu

Mwanablogu Some Thoughts from Tunisia, kwa upande wake, alielezea kilichomtokea wakati alipokwenda kupiga kura katika masaa ya mwisho wa siku hiyo:

كيما قلت سبقني مرافقي للقاعة متاع الانتخاب وكيف دخلت انا نلقا الدنيا داخلة بعضها والجماعة يتغامزو عليه ويتلفوا في الجرّة (ما فاقوش اللي احنا مع بعضنا). اكهو فهمت آش صار: ضهر السيّد مازال في دارو وهوما ريڨلولو اموروا وانتخبوا في بلاصتوا وصححوا في الدفتر في بلاصتوا… آيا قالولو ما صار شيء برّا للخلوة اختار وموش لازم تصحح (الورقة كلها مصححة وماعادش فمة بلايص)… هاذا كلّو صاير وانا واقف نتفرّج!! السيّد مشى للخلوة وانا نسمع فيهم يْوَشْوْشُو ويحكيو بالسرقة بالحرف الواحد:
“هذا العمدة انتخب في بلاصتوا…!!!!”

Kama nilivyosema, mwenzangu alikwenda kwenye kituo cha kupigia kura kabla yangu. Wakati nilipoingia chumbani, niliwaona wale waliokuwepo wamechanganyikiwa na wangine walikuwa wakipepeseana macho wakijidai kana kwamba hakuna lolote lililotokea (hawakugundua kwamba tulikuwa pamoja). Haraka nikaelewa kila kitu: wakati bado yule bwana akiwa nyumbani kwake, walikwishapiga kura na kusaini badala yake.
Halafu wakamwambia: “hakuna kilichotokea Unaweza kuchagua wagombea wako na hauhitajiki kusaini. (Karatasi lote lilikuwa limesainiwa na hapakuwa na nafasi kwa saini nyingine).
Haya yote yalitokea wakati nikiwa nimesimama pale. Mwenzangu alikwenda kupiga kura na nikawasikia wananong’ona:
“Omda” (chifu wa jamii) alipiga kura badala yake.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.