Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Machi, 2010
Lebanoni: Wafanyakazi wa Ndani Wanaotoroka
“Mfanyakazi wa ndani anapotoroka kutoka kwenye nyumba ya mwajiri wake, kituo cha polisi hakiwezi kufanya lolote kwa sababu hakuna sheria dhidi ya wafanyakazi wa ndani wanaotoroka. Kwa hiyo ofisa wa...
Misri: Wafanyakazi wa IslamOnline Wagoma
Mamia ya wafanyakazi, wahariri, na waandishi wa habari walianza mgomo wa kuonyesha hasira yao katika mtandao unaosomwa sana wa jiji la Cairo unaojulikana kwa jina la Islamonline baada ya kuwa wafanyakazi wapatao 250 wamefukuzwa kazi. Kwa mara ya kwanza, wagomaji wanatumia kwa ufanisi na vizuri kabisa aina mpya ya chombo cha habari ili kuvuta usikivu na uungwaji mkono katika kile wanachokipigania, kuanzia na Twita inayoendelea mpaka mmiminiko wa habari wa hapo kwa hapo.
Moroko: Wafanyakazi wa Shirika la Misaada La Kikristu Wafukuzwa
Wiki iliyopita, wafanyakazi 20 wa Kijiji cha Matumaini, makazi madogo ya yatima katika mji mdogo wa Moroko vijijini, waliondolewa (walifukuzwa) nchini bila onyo, kwa madai ya kuhubiri dini.
Iraki: Ni Siku ya Uchaguzi Kwenye Twita
Ni siku ya uchaguzi nchini Iraki na ulimwengu wa Twita umekuwa uking’ong’a na habari mpya mpya tangu mapema asubuhi. Waandishi wa habari na wanahabari wa kijamii walijaribu kutumia Twita ili kutupasha habari kuhusu mambo yanavyotukia nchini humo.