Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Mei, 2014
Sisi Ashinda Uchaguzi wa Rais Misri; Mpinzani Pekee Sabahi Ashika Nafasi ya Tatu
Jenerali Abdel Fattah Al-Sisi ameshinda urais kwa kishindo, huku akimbwaga mpinzani wake wa pekee Hamdeen Sabahi, ambaye ameshika nafasi ya tatu. Baada ya siku tatu za zoezi la upigaji kura, Sisi ameshinda kwa asilimia 93.3 ya kura zote. Hamdeen alipata asilimia 3 wakati asilimia 3.7 zimeharibika.