· Januari, 2013

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Januari, 2013

Uchafuzi wa Hewa wa Kutisha Jijini Tehran Waanikwa

  22 Januari 2013

Uchafuzi wa hewa umekuwa adui wa umma kwa mamilioni ya watu wa Tehran kwa miaka mingi sasa. Mapema mwezi huu, Wizara ya Afya ilitangaza kuwa, mwaka uliopita, zaidi ya watu 4, 400 walipoteza maisha kwa sababu ya uchafuzi wa hewa huko Tehran, mji mkuu wa Iran.

Mwaka Mpya na Mienendo ya Zamani Nchini Bahrain

  8 Januari 2013

Wakati nchi mbalimbali ulimwenguni kote zikiukaribisha mwaka mpya kwa fataki na shamrashamra, serikali ya Bahraini iliandaa utaratibu wa aina yake kwa waandamanaji nchini humo. kwa bahati, watumiaji wa mtandao wa intaneti walikuwa tayari, kuonesha na kuweka kumbukumbu ya baadhi ya matukio kwa ajili ya kushuhudiwa na sehemu nyingine yote ya ulimwengu.

Hakuna Usalama kwa Waandishi wa Kiraia Nchini Bahrain

  1 Januari 2013

Baada ya video ya "kibao" cha polisi wa Bahrain kusambaa sana mtandaoni, Waziri wa Mambo ya Ndani alitoa tamko akiomba kuwa yeyote aliyepiga picha tukio hilo aliripoti haraka kwa mamlaka zinazohusika. Siku mbili baadae, na kinyume na kauli hiyo, watu wengi walishangazwa na kukamatwa kwa mpiga picha.