Nchini Misri, udhalilishaji wa kijinsia ni tatizo kubwa, na ndilo jambo linaloongozwa kupingwa na Wamisri. Maandamano yalifanywa na vijana wadogo wa Misri, wasichana kwa wavulana katika mji mdogo wa Nasr jijini Cairo mnamo tarehe 4 Julai kwa lengo la kutuma ujumbe kupinga udhalilishaji wa kijinsia.
Tangu mapinduzi yalipofanyika, Wamisri wanaotumia mtandao wa intaneti na wasiotumia mtandao wa intaneti wamekuwa wakisimama imara kupinga udhalilishaji wa kijinsia pamoja na machafuko yatokanayo na kutokujali usawa wa binadamu. Mwezi Juni matembezi ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia yalishambuliwa. Haikujalisha, harakati za kukabiliana na udhalilishaji huo zinaendelea.
Malengo ya maandamano ya Julai 4 yalilenga kuweka msimamo kuhusu kupinga udhalilishaji wa kijinsia na kudai usalama wa mitaa kwa wote. Maged Tawfiles alikuwepo kwenye tukio na alipiga picha zifuatazo (picha zote zimetumika kwa ruhusa):