Omar Qatifaan, Mwanaharakati wa Habari mwenye umri wa miaka 14, aliuawa Mei 21, 2013 wakati alipokuwa anaripoti mapigano kati ya Jeshi la Syria na waasi wanaopinga serikali ya nchi hiyo kusini mwa al-Ballad eneo la Syria karibu na mpaka na Jordan.
Nyaraka kuhusu Syria zilizotolewa na Mradi wa vyombo vya habari vya vijana ziliripoti kuhusu kifo chake, na blogu ya habari nchini humo YALLA SOURIYA ilimwita kijana huyo kuwa “Roho wa Syria”.
Mgogoro wa Syria, kama vile Mapinduzi mengine yaliyozikumba nchi za Kiarabu, zimesababisha kuongezeka kwa waandishi wa habari za kiraia wanaoripoti kutoka katika kwenye uwanja wa vita kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya majeshi yanayounga mkono serikali na yale ya waasi. Wengi wamekuwa kizuizini, kuteswa, na hata kuuawa wakiwa katika jitihada za kuutangazia ulimwengu habari za mapinduzi.
Watoto pia wameumia kupindukia wakati wa vita, na maelfu wakiuawa wakati wa ghasia hadi wakati huu.
Mwanaharakati mwingine wa vyombo vya habari alirekodi video ya Qatifaan mara tu alipouawa. Video hiyo iliwekwa kwenye YouTube na SyrianDaysOfRage: [NI VIDEO INAYOTISHA]: