Misri yasema: “HAYAKUWA mapinduzi ya kijeshi”

Makala haya ni sehemu ya habari zetu maalumu  Wamisri wamwondoa Morsi

Hatua ya Marekani kuingilia masuala ya ndani ya Misri – habari zinazotangazwa mashirika ya habari, hususani CNN, kuhusu siasa zinavyoendelea Misri – zilikumbana na moto jana usiku. Kung'olewa kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi baada ya kudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu madarakani kuliamsha shamra shamra nchi nzima, pamoja na vurugu kati ya wafuasi na wapinzani wa Morsi.

Wakati mashabiki wa Morsi wakisema kwamba hatua ya kuondolewa kwa Morsi madarakani ilikuwa ni mapinduzi ya kijeshi, kambi ya wapinzani wa Morsi inasisitiza kuwa yale yalikuwa ni matakwa ya watu, yaliyoungwa mkono na jeshi imara la nchi hiyo lililorahisisha kumwondoa Morsi.

Wengi pia wana hasira kwa kile wanachokiita hatua ya Marekani kuingilia mambo ya ndani ya Misri. Wanasema kuwa “kauli ya kukera” iliyotolewa na Rais wa Marekani Barak Obama iliupuuza umma wa watu walioamua kuingia mitaani kudai uhuru wao na badala yake kurukia masuala ya misaada. Taarifa ya Marekani, iliyotolewa Julai 3, inasema:

Marekani inafuatilia mwenendo wa mambo nchini Misri, na tunaamini kwamba hatimaye mustakabali wa Misri unaweza kutengenezwa na watu wa Misri wenyewe. Hata hivyo, tunatiwa wasiwasi na uamuzi wa Jeshi kumwondoa Rais Morsi na kusimamisha katiba ya nchi hiyo. Ninalitaka jeshi la Mirsi kuchukua hatua za haraka na za kiwajibikaji kurudisha mamlaka kamili kwa serikali ya kiraia iliyochaguliwa kwa njia za kidemokrasia mara moja kwa njia za wazi na za pamoja, na kukwepa kumkamata Rais Morsi na wafuasi wake. Kwa kuangalia mwenendo wa mambo leo hii, nimezielekeza idara na mashirika yanayohusika kutathmini matokeo ya matukio haya chini ya sheria yetu ya Marekani inayoongoza misaada yetu kwa serikali kwa Misri.

Kufuatia tamko hilo, CNN, ambayo kwa sasa inatangaza moja kwa moja yanayoendelea Misri, ilianza kile kinachoitwa na raia wa mtandaoni kuwa “kampeni ya ghafla ya kumwuunga mkono Rais wa Muslim Brotherhood aliyeng'olewa na uhalali wake kwa kuielezea mikutano ya wafuasi wa Morsi kuwa “yenye amani”, wakiyaita madai ya wengi “mapinduzi ya kijeshi” na wakipinga hatua za kijeshi dhidi ya waandamanaji “wasio-na-vurugu” wa Muslim Brotherhood :

@:CNN Vurugu zalipuka wafuasi wa Morsi walipopinga mapinduzi ya kijeshi http://on.cnn.com/11nnpPL

The new logo of the CNN - Photo Posted by  ‏@aelsadek

Nembo mpya ya CNN – Picha imewekwa mtandaoni na ‏@aelsadek

Nembo mpya ya Sadek, kwa CNN, ikiwa na nembo ya Muslim Brotherhood. Maandishi ya Kiarabu ni kauli mbiu yao: Beba silaha

Wael akiandika maoni kujibu uongo wake:

@Waelucination Maandamano ya amani? Acheni kudanganya @CNN pic.twitter.com/y9AamNfKXF

The Muslim Brotherhood "peaceful" rallies. @Waelucination argues that the CNN is lying in its portrayal of the pro-Morsi protestors

The Muslim Brotherhood “peaceful” rallies. @Waelucination anasema CNN inadanganya katika picha yake ya waandamanaji wa wafuasi wa Mursi. Picha hii inaonyesha uwepo wa wanajeshi wenye silaha miongoni mwa waandamanaji

Kuhusu kutokupendelea kwa CNN wakati wa kutangaza mapigano yaliyoanzishw ana wafuasi wa MB, May Kamel aligusia:

@MayKamel Wakati huu ambapo MB wamekuwa magaidi na wanashambulia watu kwenye viwanja vya Tahrir kwa silaha, matangazo ya moja kwa moja ya CNN hayaoni sababu ya kuonyesha hali hiyo #CNN_STOP_Lying_About_Egypt

Akiwa ameudhiwa na majibu ya utawala na mashirika ya habari ya Marekani, raia wa mitandaoni walianzisha alama habari #not_a_coup & #MindYourOwnBusinessUS kwenye mtandao wa twita.

not a coup

Waleed anasema:

@WilloEgy raia milioni 33 waliingia mtaani walimtaka #Morsi aachie madaraka na bado mnaita ni mapinduzi ya kijeshi? Mnapindisha ukweli kwa makusudi.

Wakati Ahmed Sabry alisema:

@A_M_Sabry hatukuwahi kumchagua #Obama kuitawala Misri…nadhani #MindYourBusinessUS

Baheya anaongeza:

@Baheyah: Ni Mpinduzi ya Wamisri na sio ya Kijeshi, Wamisri walitaka kumtoa Mosri kwa kutumia silaka zao za maangamizi = SAUTI yao

Katika posti yake, yenye kichwa cha habariJuni 30: Mpango Halisi, Yusra Badr anasema mwaka mmoja wa utawala wa Muslim Brotherhood umelinyima taifa la Misri sherehe zilizosubiriwa kwa muda mrefu na kuzigeuza kuwa maombolezo. Anaongeza:

Mimi si mwanaharakati wa kisiasa, mimi si mwandishi na wala si mchambuzi kitaaluma, lakini ni mmoja wa mamilioni ya Wamisri walimtaka Mosri afungashe virago kutoka Ikulu. Ni mmoja wapo wa mamilioni ambao mioyo yao inauma kwa kunyimwa ushindi tulioupata Juni 30 kwa kuchezea ukweli na kuchanganya ulimwengu ili kuufanya utudharau.

Anahitimisha:

Kwa hiyo muelewe, kwa maneno rahisi, huenda hata ya kijinga, kwa sababu ninaadika usiku wa manane na sikutumia marejeo yoyote. Lakini marejeo hayana umuhimu kwangu kwa sababu nimekuwa nikiishi kwenye zimwi hili kwa mwaka sasa, na ninajivunia kile tulichokifanya Juni 30 na kwa kuungwa mkono na jeshi.
Ndiyo hivyo; mpango halisi. Haya si Mapinduzi ya kijeshi, haya ni matakwa ya taifa yanayohalisishwa kwa mbinu isiyo na utata wowote

Makala haya ni sehemu ya habari zetu maalumu  Wamisri wamwondoa Morsi

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.