Misri: Wafuasi wa Morsi Wapambana na Waandamanaji Wanaompinga Morsi

Makala haya ni sehemu ya habari zetu maalamu  Wamisri Wamwangusha Morsi

Mapambano yaliyotarajiwa kati ya wafuasi wa Muslim Brotherhood na waandamanaji waliotaka rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi aondoke yametokea leo [June 6, 2013]. Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza na ulionekana moja kwa moja kwenye televisheni, na ulirushwa kwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya ndani na vile vya kimataifa. Watu wasiopungua 17 waliuawa na zaidi ya waandamanaji 400 wakijeruhiwa katika mapigano nchini kote Misri leo, tukio ambalo mitandao mingi ya kijamii inalielezea kama “lililotarajiwa” na “linalosikitisha.”

Ayman Mohyeldin, mwandishi wa kigeni wa kituo cha televisheni cha NBC News anayeishi Misri, anatwiti:

@AymanMMaelfu ya wafuasi wa Morsi waliandamana wakipita daraja la Octoba 6 wakielekea tahrir. Helkopta ya kijeshi iliruka angani

The frontline of clashes on the Nile corniche. Photograph shared by @SherineT on Twitter

Mapambano ya mwanzo katika njia iliyoko pembezoni mwa mto Nile. Picha imewekwa kwenye mtandao wa twita na @SherineT

Mwandishi wa kituo cha televisheni cha Al Jazeera wa Cairo Sherine Tadros anaongeza:

@SherineT: Ghasia tupu hapa Maspero. Maelfu wanapambana na maelfu. Vita vya mtaani. Watu waliojeruhiwa wamelala chini

Maspero ni jengo la televisheni na redio ya taifa ya Misri lililoko katikati ya Cairo, na liko mita kadhaa kutoka viwanja vya Tahrir, amahali ambapo waandamanaji wanaompinga Morsi wanaendelea na sherehe za kuondoka kwa Morsi.

Na Andy Carvin anabainisha:

@acarvin: Video ya kusikitisha inaonyeshwa kwenye kituo cha al jazeera hivi sasa -ikiwaanesha jamaa kadhaa wakirusha mawe, kila mmoja akimwulika kwa toshi ya kijani ili kupata shabaha kwa wapinzani wao

Haya hayatokei ndani ya Cairo pekee. Nje ya Cairo, mapigano wameripotiwa.

Mostafa Hussein anaandika:

@moftasa: Vita vya mtaani vinaendelea mjini Alexandria. Habari zinaonyeshwa kwenye televisheni ya Al Arabiya.

Thousands of pro-Morsi protestors cross the October 6 bridge. Photograph shared by @AymanM on Twitter

Maelfu ya wafuasi wa Morsi wakivuka daraja la Oktoba 6 mapema leo. Picha imewekwa kwenye mtandao wa twita na @AymanM

Mohamed Fadel Fahmy anaongeza:

@Repent11: Mwandishi wa habari akiwa Suez amenipigia sasahivi akisema kuna mapigano ya kutisha yanaendelea kati ya jeshi na waandamanaji wanaomwunga mkono Morsi. Milio ya risasi inasikika na kuna majeruhi wengi.
Na Ahmed Mwaheb, kutoka Ismailia, anauliza [ar]:

احا الجيش فين #الاسماعيلية في حرب شوارع و الاخوان معاهم كل انواع الاسلحة

@AhmedMwaheb: Liko wapi jeshi? Kuna vita vya mitaani hapa Ismailia na wafuasi wa Muslim Brotherhood wa kila aina ya silaha

Mapigano hayo, yaliyotarajiwa na yanayoogopwa na wengi yametokea siku mbili baada ya Morsi, mgombea wa chama cha Muslim Brotherhood aliyeshinda urais mwaka mmoja ulippita, kung'olewa madarakani na jeshi kufuatia maandamano makubwa yakimtaka ajiuzulu kumaliza utawala wa chama cha Muslim brotherhood nchini Misri.

Lawama nyingi zinaelekezwa kwa jeshi, utawala wa zamani na chama cha Muslim Brotherhood kwa mapigano hayo.
Philip Rizk anasema:

@tabulagaza: Jeshi/itawala wa zamani pamoja la Muslim Brotherhood wanastahili kubeba lawama kwa mapigano haya mabaya ya kutumia bunduki yanayoendelea karibu na tahrir. Chuki inaongezeka kwa pande zote kwa kila risasi inayorushwa

Na Mohammed Maree anahitimisha:

الإخوان لن تقوك لهم قيامة بعد ذلك ، بعد هذة الدماء التى سالت ستحل جماعتهم ولن يمارسوا العمل السياسى

@mar3e: Muslim Brotherhood hawatakuwa na mustakabali mzuri tena. Damu inayomwagiga ndiyo imekisambaratisha chama hicho na kinajizika chenyewe kwenye medani za siasa

Mapigano yanaendelea wakati makala haya yakiandikwa.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.