Rais wa Zamani wa Misri Morsi Aibukia Kwenye Mtandao wa Twita

Rais Mohamed Morsi si rais wa Misri tena. Badala yake, analalamika kwenye akaunti yake ya twita iliyothibitishwa @EgyPresidency.

Utawala wa mwaka mmoja wa Morsi ulifupishwa, baada ya maandamano makubwa Misri kote kumtaka ajiuzulu kuanzia Juni 30.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Abdel Fattah Al Sisi alisema kwenye tangazo lake lililorushwa moja kwa moja na televisheni dakika chache zilizopita kwamba Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba Adly Mansour atakuwa rais mpya wa mpito na kwamba serikali ya umoja wa kitaifa itaundwa.

Al Sisi vile vile alitangaza kwamba katiba ya Misri imesimamishwa na kwamba maandalizi yatafanywa kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na Wabunge.

Katika mfululizo wa twiti, kwa Kiingereza, Morsi ameelezea kitendo kilichofanywa na Jeshi kuwa ni mapinduzi kamili ya kijeshi kumpindua:

@EgyPresidency: Rais Morsy: Hatua zilizotangazwa na uongozi wa Jeshi zinamaanisha mapinduzi kamili ya kijeshi yasiyokubalika na watu wote walio huru katika taifa letu

Anaongeza:

@EgyPresidency: Rais Morsy: Tangazo la Jeshi linakataliwa na watu wote walio huru waliojitahidi kuleta demokrasia ya kiraia nchini Misri.

Na anabainisha:

@EgyPresidency: Rais Mosry anawasihi wananchi na wanajeshi kuheshimu sheria na katiba na kutokukubali mapinduzi haya yanayoirudisha nyuma

Morsi anatoa wito wa kuepusha umwagaji wa damu:

@EgyPresidency: Rais Morsy anamsihi kila mtu kutunza amani na kuepuka kumwaga damu ya mwananchi mwenzake.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.