Iran: Je, Ufunguo wa Rais Mpya “Utafungua” Tatizo Lolote?

A key, the symbol for Rouhani's campaign

Alama ya kampeni za Rouhani ilikuwa ni Ufunguo. Picha kupitia Mashreghnews

Alama ya Rais mteule Hassan Rouhani ilikuwa ni ufunguo. Kwa sasa, raia wa mtandaoni wa Iran wanajadili kama Rouhani ataweza kufungua kila kufuli. Rouhani aliahidi kuleta serikali “yenye tumaini na iliyo makini” na hivyo, maelfu ya watu wa Iran walisherehekea ushindi wake wakitegemea mustakabali mzuri wa maisha ya baadae.

Kwenye blogu ya Omid Danaameandika:

Ufunguo la Rouhani utafungua kufuli gani? Mostafa Tajzadeh [ mwanamapinduzi aliyefungwa gerezani] anasema kuwa, kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa ni jambo ambalo halipo mikononi mwa Rouhani. Khatami hakusema kuwa tupunguze kiwango cha matarajio yetu? Mara nyingi watu wanasema, kwa malengo mazuri, namna ya kuelekea kwenye muafaka wa matumizi ya nyuklia, uhusiano na Marekani pamoja na mgogoro wa Syria vipo ndani ya uwezo wa Rais… pamoja na yote haya kusemwa, funguo za Rouhani ni za kufungulia milango ya nyumba yake au ofisi yake tu.

Jaleboon anaandika:

Baadhi ya watu, kama ilivyo kwa Omid Dana, anauliza ni makufuli gani anavyoweza kuyafungua Rouhani. Jibu ni kuwa, ameshafungua kufuli la uchaguzi uliokuwa batili kufuatia mgogoro wa mwaka 2009.

Watumiaji kadhaa wa mtandao wa intaneti wametaja matatizo ambayo wanafikiri kuwa ufunguo wa Rouhani unaweza kuyafungua.

Mahsa tweeted:

Bila kujali uhuru umefichwa au la, ninachohitaji ni kuona siku moja kuwa mfumuko wa bei za bidhaa na kukosekana kwa ajira vinapungua ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa watu wa hali ya chini hawajihusishi na uuzaji wa madawa ya kulevya..

Negar Mortazavi alitwiti:

“Vyanzo vya habari vilivyo karibu na #Rouhani vinasema kuwa, Rais huyu mteule amepanga kutuma wawakilishi maalum katika nchi kadhaa kwa lengo la kurejesha uhusiano mzuri pamoja na kuanzisha ukurasa mpya na nchi ya Tehran.

Wakati huohuo, kampeni kadhaa zinamtaka Rouhani kuboresha mtandao wa intaneti wa Iran ikiwa ni pamoja na kukomesha uchujaji wa taarifa katika mtandao wa intaneti. Kampeni ya Facebook ilimtaka Rouhani kukomesha uchujaji wa taarifa katika mtandao wa Facebook, na kikundi cha wanablogu na wanaharakati wa sayansi ya mfumo wa mawasiliano na udhibiti wake walimwandikia barua Rais mteule wakimtaka aongeze kasi ya mtandao wa intaneti. Pia, walilalamikia kuchujwa kwa taarifa za mtandaoni na pia walimkumbusha Rouhani kuwa alitumia mtandao wa intaneti katika kufanikisha kampeni yake.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.