Raia wa Misri Wamng'oa Morsi Madarakani

Mohamed Morsi, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Brotherhood siyo tena Rais wa Misri. Morsi ameng'olewa madarakani baada ya kutumikia kwa mwaka mmoja kama Rais mara baada ya maandamano makubwa nchini kote Misri yaliyomtaka kujiuzulu, maandamano hayo yalianza mapema mwezi Juni 30.

Mkuu wa majeshi ya Misri, Generali Abdel Fattah Al Sisi, katika matangazo ya mojakwa moja dakika chache zilizo pita, alisema kuwa, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba ndiye atakayekuwa Rais mpya wa mpito na kwamba serikali ya kitaifa ya Kiteknokrasia itaundwa.

Pia, Al Sisi alitangaza kuwa, katiba ya Misri imesimamishwa kwa muda na kwamba matayarisho ya chaguzi za Rais na wabunge yanaendelea.

Wengi wanafurahi kushuhudia siku za mwisho za uongozi katika siasa wa chama cha Muslim Brotherhood. Rasha Abdulla anaeleza:

Al Sisi announcing the end of Morsi's rule. Screen grab from CNN International

Al Sisi akitangaza mwisho wa uongozi wa Morsi. Picha imepigwa kutoka katika kituo cha televisheni cha kimataifa cha CCN

@RashaAbdulla: MISRI IMELETA ANGUKO LA MUSLIM BROTHERHOOD. HISTORIA IMEANDIKWA.

Raia wa Misri, Hossam Eid atamka kuwa [ar]:

مافيش اخوان تاني

@EidH: hakutakuwepo tena na MuslimBrotherhood

Na katika kuisitisha katiba kwa muda, mwanablogu Eman AbdElRahman, kwa kejeli anasema:

الى مزبلة التاريخ ياأعظم دستور في العاااااالم

@LastoAdri: Katiba kuu kuliko zote duniani, yatupwa kwenye jalala la historia.

Akitaarifu kutokea uwanja wa Tahrir Square, ambapo ndipo palipo na kiini cha mapinduzi ya Misri katika mji wa kibiashara wa Cairo:

@Beltrew: Sikuwahi kuona kitu kama hiki: wimbo wa Beladi beladi beladi unaimbwa na makundi ya watu; milipuko ya mafataki #Misri

Kwa upande mwingine wa shilingi, tamko hili liliwaghadhabisha wafuasi wa Morsi. Mosa'ab Elshamy anataarifu:

@mosaabrizing: Kuna hali ya ghadhabu katika mkutano wa Muslim Brotherhood. Kwa mbali inasikika milio ya bunduki.

Waarabu wanafuatilia kwa karibu kabisa hali ya mambo ilivyo nchini Misri.

Yemeni Abdulkader Alguneid anatwiti:

@alguneid: #Misri Hivi sasa, jeshi linamuondoa madarakani Morsi

Bahraini Salma anatamka kuwa:

جميلة يا #مصر

@salmasays: Misri ni nzuri

Mansoor Al-Jamri, pia kutoka Bahrain anakumbushia:

المصريون يصححون المسار وينهون حالة الاختطاف التي تعرض لها الربيع العربي. تحي مصر.

@MANSOOR_ALJAMRi: Raia wa Misri wanasahihisha njia waliyopitia na kusitisha utekaji nyara wa chimbuko la waarabu. Naitakia Misri maisha marefu!

And Moroccan Ahmed alikuwa na maoni tofauti:

مصر في طريقها لتصبح باكستان.. إنتخابات ونقلاب .. إنتخابات وإنقلاب … إنتخابات انقلاب.. والنتيجة: كفر بالديموقراطية وتطرف ديني وسياسي

@blafrancia: Misri inaelekea kuwa kama Pakistani. Uchaguzi na kisha mapinduzi ya serikali, uchaguzi na kisha mapinduzi ya serikali. Matokeo yake ni hali ya kutokuaminika kabisa kwa demokrasia, dini na siasa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.