· Aprili, 2013

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Aprili, 2013

Uturuki: Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya AkinaMama Waandamanaji

Wafungwa wa kisiasa wa Kikurdi wamefikia siku yao ya 55 ya mgomo wa kula. Kuna mamia ya wafungwa wa kisiasa walio kwenye mgomo wa kula nchini Uturuki, na hii imesababisha maandamano mshikamano katika bara la Ulaya, na hususani ndani ya Uturuki. Mapema jana [4 Novemba 2012], wanawake ambao ni mama wa baadhi ya wafungwa wa kisiasa walifanya maandamano ya kukaa, na walijikuta wakipambana na mabomu ya machozi, pamoja na kunyunyuziwa maji ya kuwasha. Wa- Kurdi duniani kote wanapinga kimya kinachotumika kushughulikia adha yao.

Syria: Kutwiti Kutokea Vitani Jijini Aleppo

Mwandishi wa Habari Jenan Moussa amerudi mjini Aleppo, nchini Syria, akitwiti tajiriba yake wakati vita kati ya vikosi vinavyopinga serikali na vile vinavyoiunga mkono serikali inavyozidi kushika kasi. Twiti za Moussa ni za kawaida na za kibinafsi sana, zikiwapa wasomaji wake taswira ya maisha yalivyo kwa wale walio kwenye uwanja wa vita.

Bahrain: Nani Aliyesikia Milipuko ya Bomu na Nani ni Waathirika?

8 Aprili 2013

Wakuu wa Serikali nchini Bahrain wametangaza leo kwamba wafanyakazi wawili wa kigeni wameuawa na wa tatu akijeruhiwa vibaya katika milipuko mitano tofauti kwenye maeneo ya Gudaibiya na Adliya, kwenye mji mkuu Manama. kwenye mtandao wa twita, habari hizi zilipokelewa kwa mashaka, kutokuamini na kusababisha mwito kwa utatuzi wa kisiasa wa kumaliza hali ya ghasia katika nchi hiyo, kufuatilia kusambaa kwa maandamano ya kuipinga serikali yaliyoanza terehe 14 Februari, 2011.