Bahrain: Nani Aliyesikia Milipuko ya Bomu na Nani ni Waathirika?

Makala haya ni sehemu ya Habari zetu maalum za Maandamano ya Bahrain 2011/12.

Wakuu wa serikali huko Bahrain walitangaza leo kuwa wafanyakazi wawili wa kigeni wameuawa na mtu wa tatu akijeruhiwa vibaya katika milipuko mitano tofauti ya mabomu katika maeneo ya Gudaibiya na Adliya, katika mji mkuu wa Manama.

Kwenye mtandao wa twita, habari zilipokelewa na wasiwasi na mashaka pamoja na wito wa kupatikana kwa ufumbuzi wa kisiasa kumaliza machafuko katika nchi, kufuatia maandamano kuenea dhidi ya serikali ambayo yalianza Februari 14, 2011.

Mwandishi wa habari Adel Marzooq alitwiti akiwa uhamishoni [ar]:

٥ تفجيرات وهمية واعلان مقتل الاسيويين ليس عبثيا، يريدون امتصاص الادانات الدولية لقرار منع التظاهر والمسيرات وتحويلها لادانة الارهاب

@adelmarzooq: Milipuko mitano isiyo halisi na tangazo kwamba Wa-Asia wameuawa sio taratibu. Wao wanataka kupunguza lawama za kimataifa kwa uamuzi wa kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kampeni na kuifanya ionekane kuwa ni kitendo cha ugaidi

Ahmed Habib anauliza:

اذا كانت الانفجارات استهدافا للأجانب فهم بكثرة في القرى ولم يتعرض لم أحد فما الداعي للذهاب للعدلية وام الحصم؟!

@ahmdhabib: Kama milipuko ilikuwa ikiwalenga wageni, wao ni wengi katika vijiji na hakuna mtu aliwashambulia wakiwa kule. Sasa kuna sababu gani kwenda kwa Adliya na Umm Al Hassam [maeneo ya mji mkuu Manama]?

Na Mansour Al Jamri, mhariri mtendaji wa gazeti Al Wasat, anaandika:

نأمل من وزارة الداخلية ان تنشر في مؤتمرها الصحفي اسماء وجنسيات القتلى والجرحى، اذ من حق وسائل الاعلام معرفة التفاصيل. وشكرا.

@MANSOOR_ALJAMRi: Tunatumaini kwamba Wizara ya Mambo ya Ndani itatangaza katika mkutano wa vyombo vya habari  majina na uraia wa wale waliouawa na kujeruhiwa. Ni haki ya vyombo vya habari kujua maelezo. Asanteni

Abu Omar Al Shafiee anauliza:

هل هناك أخبار عن الاسيويين الذين تعرضوا لحادث دس من قبل احد الدوريات الامنية قبل أيام ؟ هناك روائح كريهه تختق الاجواء هذة الايام ؟

@ALSHAF3EE: Je, kuna habari kuhusu Wa-Asia ambao waliofuatiliwa na doria ya polisi siku chache zilizopita? Kuna harufu mbaya inayotukosesha amani siku hizi

Hussain Yousif, mpinzani wa kisiasa anayeishi uhamishoni, anaongeza:

من حق الشعب ان يتسائل عن مصير التحقيق في دهس مركبة تابعة للداخلية آسيويين بين العكر والمعامير في #البحرين، حيث القاتل معروف


@hussain_info
: Watu wana haki ya kujua kilichotokea kwenye uchunguzi wa gari ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo iliwafuatilia Wa-Asia kati ya Ekeri na Maameer kwani muuaji anafahamika wazi

Na Sayed Ahmed Al Alawi anatia zaidi shaka:

الشخص الذي عرض على أنه قتيل الانفجار إذا كان موته بسبب ركله للقنبلة محلية الصنع كيف سيصل التفجير لرقبته دون رجله وبطنه وصدره عجيبه هالقنبلة

@SAalalawi: Mtu aliyeonyeshwa kuwa ndiye aliyeuawa katika mlipuko alikufa kwa sababu alipiga teke bomu lililotengenezwa kienyeji. Ilikuwaje mlipuko uathiri shingo yake wala si miguu yake, tumbo na kifua. Hii ni moja ya bomu lisilo la kawaida

في أحد سمع التفجيرات؟ بأذونه؟ لاترد على هالسؤال إذا ماسمعت/سمعتي بأذونك/ج

Sabeeka Al Shamlan alijibu mapigo, kwa kusema:

@Sabeeka_A: Tumerudi kwenye sifuri tena. Oh subiri, nani ambaye alisema sisi hata tumepiga hatua?

Na kisha anauliza [ar]:

في أحد سمع التفجيرات؟ بأذونه؟ لاترد على هالسؤال إذا ماسمعت/سمعتي بأذونك/ج

@Sabeeka_A: Kuna mtu yeyote aliyesikia milipuko? Kwa masikio yao wenyewe? Usijibu swali hili kama wewe hujasikia milipuko, kwa masikio yako mwenyewe

Noor Bahman anachukua hatua zaidi:

@noorbahman: Bomu humwua mwathirika hapo hapo na pia kuharibu kabisa uwiano wa eneo la jirani mwathirika alipokuwepo.

Na Salma anauliza:

@salmasays: Eh .. Viko wapi vyombo vya habari vilivyo huru wakati tunapovihitaji viwepo..

Uchochezi huu una mizizi ndani zaidi. Eyad Ebrahim anaeleza [ar]:

الكل يجذب و أنا صرت ما اصدق أي أحد، لا حكومة ولا جمعيات ولا بطيخ.

@eyade: Kila mtu hudanganya na mimi simwamini mtu yeyote – sio serikali, si upinzani, hakuna mtu yeyote.

Murad Alhayki anatoa mwito wa suluhisho la kisiasa. Yeye anasema:

كل ما تأخر الحل السياسي تعقدت الأمور أكثر وصعب حلها … دماء الناس تقوض العقل

@muradalhaiki: Kadri ufumbuzi wa kisiasa unavyozidi kucheleweshwa, na ndivyo masuala yanavyozidi kuwa magumu na ndivyo inavyozidi kuwa vigumu kuyatatua. Damu ya watu ni wito kwa matumizi ya hekima

Makala haya ni sehemu ya Habari zetu maalum ya Maandamano ya Bahrain 2011/12.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.