Mwandishi wa Habari Jenan Moussa amerudi mjini Aleppo, nchini Syria, akitwiti tajiriba yake kadri vita kati ya vikosi vinavyopinga serikali na vile vinavyoiunga mkono serikali inavyozidi kushika kasi. Twiti za Moussa ni za kawaida na za kibinafsi sana, zikiwapa wasomaji wake picha kamili ya maisha yalivyo kwa wale walio kwenye uwanja wa vita.
Moussa, ambaye ni ripota wa kituo cha televisheni za kiarabu Al Aan TV, kilichopo jijini Dubai, Jamhuri ya Falme za Kiarabu, anasema:
@jenanmoussa: Ni jambo kubwa sana kurudi Allepo, kukutana na rafiki zangu. Jiji linaonekana kuwa na nafuu zaidi kuliko ilivyokuwa mara ya mwisho nikiwa hapa. Watu wameshazoea vita.
Chakula chake cha jioni, jijini Aleppo, anakipata akisikia sauti za mabomu yakidondoka jirani na aliko:
@jenanmoussa: Ni wakati wa chakula cha jioni hapa Aleppo. Tunakula kuku wa ki-Mexico wakati tukisikia sauti za mabomu yakidondoka kwa mbali,
Baada ya usiku huo akiwa jijini, Moussa anashangaa:
@jenanmoussa: Habari za asubuhi kutoka Aleppo. Sikuweza kulala mpaka saa 12 alfajiri. Kila wakati ninafunga macho yangu ninapatwa na hisia kuwa mabomu yanaanguka. Mungu, watu wanawezaje kubaki na akili zao hapa?
Jijini Aleppo, anatembelea mahali ambako kombora lilianguka siku zipatazo 45 zilizopita. Anatwiti:
@jenanmoussa: Mapema leo nilienda kwenye eneo ambako kombora la SCUD lilidondoka siku zipatazo 45 zilizopita hapa Aleppo. Miili sita bado haijapatikana.
@jenanmoussa: Jijini Aleppo nilimwona baba amekaa kwenye jabali, akitiririkwa na machozi. Alikuwa bado anatafuta miili ya mabinti zake wawili na mkewe
@jenanmoussa: Wakati nikiwa nae, baba huyo alipata malapa ya mwanae na nywele kidogo (za kike) chini ya jabali hilo. ‘Labda ni mke wangu’ aliniambia
Pamoja na hali ngumu, Moussa anafanya utani kidogo:
@jenanmoussa: Wanaharakati hapa Aleppo hunicheka. Mara nyingine mimi huwa ni mtu pekee anayevaa nguo ya kuzuia risasi nyumbani. Watu wote wameshazoea milio ya bunduki.
Na anaenda kulala bila kupata chakula cha jioni:
@jenanmoussa: Hatujala chakula cha jioni usiku huu. Hatujaoga. Hilo si hitaji la msingi katika mji kama Aleppo. Usiku mwema kwenu nyote.
2 maoni
Tuepuke mambo madogo sana kama vile ubaguzi katika mgawanyo wa raslimali unaofanya kuwepo kwa utofauti mkubwa kati ya matajiri na masikini
szkolenia zarządzanie
Syria: Kutwiti Kutokea Vitani Jijini Aleppo · Global Voices in Swahili