Uturuki: Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya AkinaMama Waandamanaji

Wafungwa wa kisiasa wa Kikurdi wamefikia siku yao ya 55 ya mgomo wa kula. Kuna mamia ya wafungwa wa kisiasa walio kwenye mgomo wa kula nchini Uturuki, na hii imesababisha maandamano mshikamano katika bara la Ulaya, na hususani ndani ya Uturuki. Mapema jana [4 Novemba 2012], wanawake ambao ni mama wa baadhi ya wafungwa wa kisiasa walifanya maandamano ya kukaa, na walijikuta wakipambana na gesi ya machozi, pamoja na kunyunyuziwa maji ya kuwasha. Vyombo vikuu vya habari na mawaziri wa serikali wote wamebakia kimya katika kuzungumzia hasira ya watu wa Kikurdi, na upuuziaji wao wa suala la makazi ya kisiasa kwa wa-Kurdi nchini Uturuki umefanya hali kuwa mbaya.

Katika maeneo mengi ya Kurdistan, kumekuwa na maandamano ya mshikamano lakini licha ya tahadhari zilizotolewa mgomo wa kutokula umepenya katika mikoa ya Kikurdi, na kwa kweli kuna vyombo vya habari vikuu vichache vinavyoripoti kuhusu mgomo huo wa kutokula. Ukosefu wa vyombo vya habari imewakasirisha Wakurdi wengi, ambao wana jadili masuala hayo katika mitandao ya kijamii. Hulya, kutoka Liverpool, anasema:

@hulyaulas: Mgomo mkubwa wa kisiasa wa kutokula katika historia kwa wafungwa wa Kikurdi unapuuzwa na haupewi nafasi yoyote katika vyombo vikuu vya habari.

Dirman anaongezea:

@dirman95: Ni vigumu kula ukijua kwamba mgomo wa kutokula umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya siku 51 na dunia haifanyi lolote kuhusu hilo … inakera.

Chombo cha habari cha Al Jazeera ndicho cha pekee kilichokubalika kama chombo cha kikuu cha habari cha kimataifa kilicho onyesha kiwango cha mgomo wa kutokula. Wao wametumia vyombo vya habari vya kijamii kuhamasisha. Kwa mfano wao hivi karibuni walitwiti:

@ajstream: Kwa nini serikali na vyombo vya habari nchini Uturuki wanapuuza mgomo wa kutokula unaofanywa na wafungwa wa kisiasa wa Kikurdi 715?

Hati ya mtandaoni ya kupinga kitendo hicho imezinduliwa, ina wafuasi 3451 hadi sasa, inayoitaka serikali ya Kituruki kushiriki katika mijadala inayojenga na wafungwa. Judith Butler from Berkeley alitoa maoni:

Serikali ya Kituruki lazima kuingia katika mazungumzo makubwa na wafungwa hawa ambao sasa wanahatarisha maisha yao ya kufichua dhuluma wanayofanyiwa.

KurdishBlogger.com aliposti picha ifuatayo kwenye mtandao wa Facebook:

Wakurdi katika Slemani, Afrika Kurdistan waonyesha mshikamano na dada na ndugu zao Wa-Kikurdi (angalau mahabusu 682 mahabusu) ambao wako kwenye mgomo wa kutokula katika magereza 67 nchini Uturuki.

Na Tara Fatehi, mwanaharakati wa Kikurdi Nchini Australia, alionyesha hasira yake dhidi ya jumuiya ya kimataifa:

Maelfu ya wafungwa wa kisiasa Kikurdi wamekuwa katika mgomo wa kutokula nchini Uturuki tangu Septemba 12 na jumuiya ya kimataifa bado iko kimya. Hii ni njaa ya wa-Kurdi kupigania uhuru, wala si dhana mpya. Wakurdi wamekuwa wakipigania haki, amani na uhuru kwa miongo kadhaa. Hannelore Kuchlersaid alilizungumzia hili vizuri “Kurdistan ni nchi ambayo imechukuliwa mateka.” na wakati vyombo vya habari vya kimataifa vyataka kukufanya ufikiri hatua hii ni kwa sababu ya Abdullah Ocalan na PKK, ukweli si huo. Suala hapa ni kuhusu kupata haki za msingi katika nchi yao wenyewe.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.