Asasi za Kiraia za Urusi “Zakaguliwa” na Mwendesha Mashitaka

Wanaharakati wa DemVybor katika jiji kuu la eneo la Voronezh waliripoti kwenye blogu ya DemVybor[ru] kwamba Asasi Zisizo ki-Serikali zinakaguliwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma wa jiji hilo. Mashirika manne yaliyolengwa ni wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Voronezh [ru]: ni Vuguvugu la Haki za Binadmau linaloendeshwa na Vijana, Kikundi cha Haki za Binadamu kinachounganisha mikoa kadhaa, Mfuko wa ECOSOCIS, Kituo cha Kukuza Mashirika yanayoanzishwa a umma. Makala ya Article20.org [ru], tovuti ya mtandao wa habari za haki za binadamu umechapisha [ru] picha ya barua ya mwendesha mashitaka wa umma iliyo kwenye fomati ya PDF iliyoandikwa kwa ECOSOCIS kuomba taarifa. Ombi hilo linasemeka:

Прокуратурой области по заданию Генеральной прокуратуры Российской Федерации проводится проверка исполнения законодательства о некоммерческих организациях и противодействии экстремистской деятельности.

Ofisi ya mwendesha mashitaka wa mkoa, kwa maagizo ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Shirikisho la Urusi, inaendesha ukaguzi wa juhudi za kuzingatia sheria katika Mashirika Yasiyo ya Serikali na ikiwa yanajihusisha na shughuli za kisiasa.

Voronezh Prosecutor's Office letterhead. Screenshot, April 7, 2013.

Sehemu ya barua ya Mwendesha Mashitaka wa Voronezh. Picha ya skiri ya komputer, Aprili 7, 2013.

Taarifa zinazohitajiwa kimsingi ni nyaraka za kifedha na kiutawala, ikiwa ni pamoja na, kiasi cha fedha kilichopokelewa na mashirika hayo kutoka nje ya nchi. Sheria mpya imesukwa kwa makusudi ili kulazimisha upokelewaji wowote wa fedha kutoka nje uwekwe wazi. Wengine wanasema, hata hivyo, kwamba imelenga kukata mirija ya misaada ya fedha za kigeni kwenda kwenye AZISE za ki-Rusi.

Kama vile haitoshi, mwendesha mashitaka anataka taarifa mahususi kuhusu shughuli hasa za mashirika hayo, swali ambalo linaonekana kulenga katika sheria ya “kuzuia uchochezi wa kisiasa”, lakini kwa wakati huo huo ikisomeka kama maelekezo kwa wahusika kusaili matumizi ya fedha zao:

15) информацию об организованных и произведенных организацией массовых публичных мероприятиях (митинги, демонстрации, шествия, пикетирования, собрания), а также о массовых мероприятиях, в которых организацией принято участие. Дайте краткий анализ массовых мероприятий, цели и результаты их проведения.

15) taarifa za matukio ya hadhara (mikutano, maandamano, matembezi, migomo, mikutano) iliyoandaliwa na kufanywa na shirika, pamoja na matukio ya umma ambayo shirika limejihusisha nayo. (Unaagizwa) kutoa uchambuzi mfupi wa matukio hayo ya umma, malengo yake, na matokeo ya kufanya hivyo.

Labda Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa umma inayataka mashirika hayo kujisaili ni kwa kiwango gani yamezingatia malengo ya kuwepo kwake! Kuna uwezekano kuwa baada ya kupeleka nyaraka zote zinazotakikana, Mashirika hayo yanayolengwa yatakuwa na mawazo bora zaidi ya namna yanavyofikia malengo yao kwa ufanisi. Itakuwa hivyo, kwa kweli, ikiwa hayatafungwa kwanza.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.