Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Aprili, 2011
Naijeria: Je, Teknolojia itaathiri uchaguzi wa mwaka 2011?
Wanaijeria wanaingia kwenye uchaguzi tarehe 16 Aprili 2011 kumchagua rais wao mpya. Uchaguzi uliahirishwa kutoka siku iliyokuwa imepangwa awali ya Aprili 9 kwa sababu ya kasoro za kimuundo. Katika makala hii tunatazama namna Wanaijeria wanavyotumia teknolojia kuwezesha uwazi katika uchaguzi, ushirikishwaji wa kisiasa na utawala bora.
Ivory Coast: Je, nani anadhibiti televisheni ya taifa ya RTI?
Bado kuna mkanganyiko kuhusu swali la nani hivi sasa ndiye mwenye udhibiti wa Radio Télévision Ivoirienne (RTI) , ambacho ni kituo cha televisheni ya taifa.
Naijeria: Maonesho ya Picha za Kampeni ya Urais
George Esiri alifuatilia kampeni za kugombea urais za chama cha PDP huko Naijeria. Maonesho ya picha alizopiga yalizinduliwa jana katika Kituo cha Yar'Adua.
Myanmar: Simulizi za Wafanyakazi wa Misaada Baada ya Tetemeko la Ardhi
Myanmar bado inasumbuka kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 ambalo liliikumba nchi hiyo. Mwandishi wetu aliyeko Myanmar anatafsiri mahojiano na simulizi za wakazi pamoja na wafanyakazi wa misaada ambao walishuhudia kiwango cha uharibifu uliofanywa na tetemeko hilo kaskazini mashariki mwa Myanmar.
Japani: Iambieni Dunia isaidie
Picha zilizotafutwa na kuwekwa kwenye twita zinaweza kuleta mambo ya kushangaza. Tafuta herufi hizi “宮城” (Miyagi) na picha chache zitatokea kutoka kwenye wilaya hiyo, moja ya maeneno yaliyoharibiwa sana nchini Japani baada ya tsunami. Nenda chini, na picha moja inaonekana, yenye rangi ya kahawia na bluu mpaka utakapoibofya…
Japani: Tsunami yaathiri eneo la pwani, yaacha kila kitu kimeharibiwa
Kufuatia tetemeko kubwa kuwahi kutokea nchini, Japani imekumbwa na tsumani mbaya zaidi iliyowahi kutokea. Watu wengi nchini kote wameganda kwenye luninga zao wakati vipande vya habari vinavyoonesha tsunami lenye urefu wa zaidi ya mita 7 kwenda juu likisomba magari na majengo.
Japan: Jijini Tokyo baada ya Tetemeko la Ardhi
Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011. Siku ya Ijumaa, Machi 11, 2011 saa 8:46:23 mchana kwa saa za Japani, , tetemeko lenye kipimo cha...
Tetemeko kubwa kuwahi kutokea nchini Japani
Siku ya Ijumaa, Machi 11, 2011 saa 8:46:23 mchana saa za Japani, tetemeko lenye vipimo vya tetemeko 8.9 liliikumba Japani, lilikiwa kubwa kuwahi kuripotiwa katika historia ya Japani.
Bahrain: Waandishi wa Habari Wazuiwa Kuingia Wakiwa Uwanja wa Ndege
Bahrain iliingia kwenye vurugu kubwa zilizoambatana na polisi kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji waliopiga kambi katika eneo muhimu la wazi linalohusudiwa sana liitwalo Lulu Jumatano iliyopita. Mchana wa siku hiyo nilipanda ndege inayotoka Doha, nchini Qatar, kwenda Bahrain, kwa upande mmoja nikitaka kujionea mwenyewe nini kilikuwa kikitokea katika nchi hii ya kisiwa ambayo ilipata kuwa nyumbani kwangu. Saa kadhaa baadaye nilijikuta kwenye ndege ya kurudi Doha, baada ya kunyimwa ruhusa ya kupita pale uwanja wa ndege.
Côte d'Ivoire: Televisheni ya Taifa RTI Inawezekana kuwa Inatangaza Kutokea Kwenye Gari la Matangazo
Kama vile alivyoelezea Julie Owono , ni vigumu kupembua mapambano ya kudhibiti vyombo vya habari vya Pwani ya Pembe (Cote d'Ivoire). Taarifa kutoka Waandishi Wasio na Mipaka inaashiria kuwa RTI...