Habari kutoka Julai, 2013
Maandamano Yasitisha Ujenzi wa Mtambo wa Nyuklia Kusini mwa China
Kufuatia siku tatu mfululizo za maandamano, inaonekana kuwa serikali ya Manispaa ya Heshan katika jiji la Jiangmen imesitisha mpango wake wa ujenzi wa mtambo mkubwa wa nishati ya Nyuklia. Baadhi ya watu wanaamini kuwa ushindi huu ni wa muda mfupi tu. Wana wasiwasi kuwa, mradi huu unaweza kuibukia sehemu nyingine karibu na Delta ya mto Pearl, Kusini mwa China mahali palipo na idadi kubwa sana ya watu.
Tanzania: Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Arusha Waipa CHADEMA Ushindi
Uchaguzi mdogo wa Madiwani Jijini Arusha umefanyika kwa amani leo Jumapili Julai 14. Mtandao maarufu wa Jamii Forums uliripoti yanayoendelea Arusha wakati wote na baada ya uchaguzi. Blogu ya Wavuti imeweka matokeo ya uchaguzi huo pamoja na picha mbalimbali za uchaguzi: Huku Tume ya Uchaguzi ikisubiriwa kuwatangaza rasmi washindi, taarifa...
Iran: Je, Ufunguo wa Rais Mpya “Utafungua” Tatizo Lolote?
Alama ya kampeni za Rouhani ilikuwa ni Ufunguo. Kwa sasa, raia wa mtandaoni wa Iran wanajadili kama Rouhani ataweza kufungua kila kifungio.
Hali ya Kidiplomasia Kati ya Zimbabwe na Nchi za Magharibi
Simukai Tinhu, mchambuzi wa masuala ya siasa anayeishi London, anauliza, “Je, mahusiano ya Zimbabwe na nchi za kimagharibi yanaimarika kadri uchaguzi unavyokaribia?”
Wakazi wa Jiangmen Nchini China Wapinga Ujenzi wa Mtambo wa Uranium
Siku ya tarehe 12 Julai, 2013, mamia kadhaa ya wakazi wa Jiangmen, jiji lililo jirani na Guangzhou ya Kusini nchini China, walifurika mtaani na kuandamana kupinga mpango wa kuanzisha mtambo wa kuchakata Urani.
Al Jazeera Yatuhumiwa Kutangaza “Habari za Upendeleo”
Al Jazeera iko kwenye wakati mgumu nchini Misri kwa kile kinachoelezwa na wengi kuwa ni "upendeleo" wake katika kutangaza habari zake wakati na baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi mnamo Julai 4. Kituo hicho cha televisheni kilichopo nchini Qatar kinatuhumiwa kuegemea upande wa wafuasi wa Muslim Brotherhood na kimegeuka kuwa mdomo wa kikundi hicho.
Kuelekea uchaguzi wa Kambodia: Matumizi ya Mtandao wa Facebook
Watumiaji wa mtandao wa intaneti nchini Cambodia wanatumia mtandao wa Facebook kwa kiwango kikubwa katika kujadili, kuendesha midahalo na kushirikishana mambo mapya yanayohusu chaguzi za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika tarehe 28 Julai, 2013. Wakati huohuo, vyama vya siasa pia vinatumia mtandao huu ulio maarufu zaidi katika kuwashawishi vijana wadogo wanaotarajiwa kupiga kura.
Uhispania: Wahalifu wa Mtandao Wavujisha Nyaraka za Chama Kinachotawala
Kikundi cha kimataifa kisichofahamika cha wahalifu wa kutumia mtandao wa intaneti wamevujisha katika mtandao wa intaneti nyaraka za akaunti za kiuchumi za chama tawala cha Uhispania za kati ya miaka ya 1990-2011
Saudi Arabia: Familia za Wanaoshikiliwa Gerezani Zaandamana
Familia za watu wa Saudi Arabia wanaoshikiliwa gerezani yaingia siku ya tatu ya kupinga kushikiliwa kwa wapendwa wao bila sababu maalum. Saudi Arabia ni moja ya nchi chache duniani ambazo bado zipo chini ya mfumo wa utawala wa kifalme na ina rekodi isiyoridhisha kuhusu haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kushikilia gerezani zaidi ya watu 30,000 bila sababu maalum.
Global Voices Yazindua Ushirikiano na Shirika la NACLA
Global Voices na Shirika la Marekani Kaskazini Linaloshughulika na Amerika Kusini (NACLA) wameanzisha ushirikiano mpya ambao utaleta kwa pamoja dira ya Sauti za Dunia ya habari za kiraia na na ile ya NACLA ya uchunguzi na utoaji wa elimu, lengo likiwa ni kuwaletea wasomaji wetu habari halisi na za kina kutoka katika eneo hili la Latini Amerika.