Uhispania: Wahalifu wa Mtandao Wavujisha Nyaraka za Chama Kinachotawala

Siku za hivi karibuni, hakimu anayesimamia kesi yaGürtel, inayohusu kashfa ya rushwa ya kisiasa nchini Uhispania inayowahusisha wanachama wa Chama cha Umma (PP), aliomba tangu mwaka 1990 kupatiwa nyaraka kufuatia mashaka ya udanganyifu wa taarifa za kiuchumi. Chama cha Umma kilikataa wakidai kuwa walipaswa kuziwasilisha hati hizo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na si vinginevyo.
Tarehe 8 Julai, 2013, mtu asiyejulikana alipakia mtandaoni hazi zenye karibu 5GB ya data za akaunti ya chama, na wakati huo huo waliweka bayana taarifa zao za kiuchumi za kuanzia mwaka 1990 katika mtandao wa anonyourvoice.com. Hati hizo zilianza kusambaa kwa haraka sana katika mitandao mbalimbali ya kijamii, kwenye torenti, blogu na katika idhaa mbalimbali. Mtu huyu asiyejulikana alizipa taarifa zilizovuja jina la utani:

Cables contables. PPgoteras. Lo que debería ser público, será público.

Accounting cables. PPleaks. Kilichopaswa kujulikana, kitajulikana tu.

Taarifa hizi, ambazo zilifichwa, kwa sasa zinapatikana kwa kila raia. Maelfu ya raia katika mitandao ya kijamii wameshaanza kuzisambaza na kuzipitia kwa umakini taarifa hizi. Unaweza kufuatilia upembuzi wa taarifa hizi katika ukurasa wa Twita kupitia kiungo ishara #CuentasdelPP [es]:

@15MayoValencia: ¿Quieres echar una mano con la #AuditoriaCiudadanaAlPP? Descarga las #CuentasDelPP, analiza y comparte! http://fb.me/L8xmiwBh
@15MayoValencia: Unapenda kutuunga mkonoDo you want to give us a hand with the #AuditoriaCiudadanaAlPP [es] [AIPP Citizen Audit]? Pakua #CuentasDelPP[es] [Akaunti za PP], zifanyie uchanganuzi na kisha uwashirikishe na wengine ! http://fb.me/L8xmiwBh [es]
@LaliSandi: Lo nunca visto: las #cuentasdelpp explotan y se esparcen a pedacitos por la red.
@LaliSandi [es]: Haikuwahi kutokea: #cuentasdelpp[es] [ Akaunti za PP] kuvuja kwa wingi na kusambaa katika mitandao ya intaneti katika vipande vidogo vidogo.
‏@alvarinaitis: #CuentasDelPP Ya en serio ¿No va a dar nadie la cara durante el día de hoy? un comunicado? nadie del @PPopular ni empresarios donantes?
‏@alvarinaitis [es]: #CuentasDelPP[es] [ Akaunti za PP] lakini ni kweli kuwa, hakuna yeyote atakayejitokeza siku ya leo? Maelezo yoyote? Hakuna yeyote kutoka @PPopular [es] Chama cha Umma (PP) au mfadhili wa Kibiashara?

Chama cha Umma(PP), ambacho kiliahidi kuleta sheria ya uwazi kabla ya siku 100 za uongozi ambapo hadi sasa bado hakijaidhinisha sheria hiyo, taarifa za kiuchumi za chama hiki zimesambaa kwa mamia ya wafuatiliaji wasiojulikana. Utawala wa umma bado unaendelea unachunguzwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.