Maandamano Yasitisha Ujenzi wa Mtambo wa Nyuklia Kusini mwa China

Kufuatia siku tatu mfululizo za maandamano, inaonekana serikali ya Manispaa ya Heshan jijini Jiangmen imetupilia mbali mkakati wake wa ujenzi wa mradi mkubwa wa mtambo wa nguvu ya Nuklia.

Baadhi ya watu wanaamini kuwa ushindi huu ulithibitishwa kwa taarifa ya maandishi [zh] iliyotolewa mapema Julai 14, 2013 – kuwa ni ya dharura tu. Watu wana wasiwasi kuwa mradi huu unaweza kuibukia sehemu nyingine yoyote, karibu na eneo lililo na idadi kubwa ya watu la Delta ya mto Pearl, Kusini mwa China.

Serikali ya Heshan iliridhia mambo kadhaa kufuatia mamia ya raia wa jiji la Heshan kuandamana Julai 12, 2013 wakipinga kujengwa kwa mradi huo ambao wanaamini utaweka maisha yao hatarini. Katika hatua ya awali, serikali ilijaribu kufikia muafaka kwa kukubali kuongeza siku za kutoa maoni ambapo iliongeza hadi kufikia siku 20. Lakini, hatua hii haikuweza kuwaridhisha raia, ambapo, tarehe 13 Julai katika mkutano na vyombo vya habari, serikali ilitangaza kuwa,“kwa kuheshimu maoni ya wananchi, mradi huu hautaidhinishwa” [zh], pamoja na kuwa utawala wa jiji ulikuwa tayari umeshaingia kandarasi ya awali na Shirika la Taifa la Nyuklia la China (CNNC).

Waandamanaji walijitokeza kwenye mitaa mbalimbali katika kupinga ujenzi wa mtambo wa Nyuklia mnamo tarehe 12 Julai, 2013. Picha kutoka Zhu Kunling weibo.

Hata hivyo, baadhi ya watu hawajaridhishwa na madai ya serikali. Kwa uzoefu, serikali za mitaa za China zimerithi mbinu ya kuchelewesha mambo kama namna ya kutuliza hasira za wananchi. Kwa mfano, huko Dailan, serikali ya jiji ilisitisha shughuli katika kiwanda cha PX mara baada ya maelfu ya watu kuandamana mwaka 2011 katika kampeni ya “Not-In-My-Back-Yard”, lakini kiwanda hicho baada ya miezi kadhaa kupita, kiliendelea na shughuli zake kama kawaida [zh].

Maoni ya “Little bee” (@小蜜蜂-V) na “Little Eaffen” (@Eaffen细细) kwenye mtandao wa Sina Weibo:

小蜜蜂-V:看了新闻发布会,但只字没提到取消两只,只是说在社会未达共识时,不立项,不动工。认误解成取消了?

“Little bee”: Katika mkutano na waandishi wa habari, msemaji wa serikali hakutaja “kusitisha”, alichosema ni ‘kwa kuwa hakujafikiwa muafaka kati ya serikali na wananchi, mradi autaidhinishwa wala ujenzi kuanza. Hivi hatukuelewa?

Eaffen细细:真的假的?不立项什么意思?应该明确表明以后都不会建才行!

Little Eaffen: Ni kweli? Ina maana gani inaposemwa ‘bado haijakubaliwa’? tunachokubaliana nacho ni ‘kutokujenga mtambo huo kabisa’!

Baadhi ya watumiaji wa mtandao walisema kuwa kusitishwa kwa ujenzi wa mtambo huo ni‘ mbinu ya kuchelewesha ’ [zh]:

张二飞flyfan:又不知道哪个内陆城市要倒霉了

Zhang Erfei flyfan: Ninajaribu kuwaza ni jiji lipi hilo ambalo halitakuwa na bahati.

就是爱摩托:会不会过几天又宣布:鹤山核燃料项目取消,经专家研究,决定将项目迁到新会~

Ninawafananisha na pikipiki: Serikali ya Heshan itatangaza kuwa hatua za ujenzi wa mtambo huo zimesitishwa, na kwa kutumia taarifa ya tafiti kutoka kwa wataalamu kuwa mradi huo utahamishwa na kupelekwa Xinhui (ambao ni jiji jingine la Guangdong)?

Hii ndio hati ambayo waandamanaji wamekuwa wakiirejelea. Imeandikwa kuwa serikali ya Jiangmen imesitisha ujenzi wa mradi huu. (Source: Sina Weibo)

Hati ya serikali kuhusiana na kusitisha mradi wa ujenzi wa mtambo wa Nyuklia[zh].

Kwa jazba na hali ya kukosa imani, mamia ya wakazi wa jiji la Jiangmen waliendelea kuandamana na kuingia siku ya tatu ya maandamano tarehe 14 Julai wakitaka kupewa hati maalum ya serikali inayoonesha kusitishwa kwa mradi huu. Wasaidizi meya wawili waliwasili mahali maandamano yalipoanzia, uwanja wa Donghu kuwahakikishia kuwa maoni yao yatazingatiwa. Hata hivyo, watu hawakuweza kukubali maneno yao matupu na badala yake, walitembea kuelekea kwenye jengo la serikali ya manispaa ambapo katibu wa kamati ya manispaa aliwaonesha hati ya kusitishwa kwa mradi huo. Walishangilia na kusema kuwa wamefanikiwa.

Hata hivyo, hati hiyo haijaondoa hali ya mashaka iliyokuwepo kwani kandarasi iliyopitishwa kati ya serikali ya Heshan na CNNC inahusisha uwekezaji wa RMB bilioni 37 (dola za kimarekani bilioni 6). Hadi sasa, CNNC hakijatangaza mabadiliko yoyote kwenye mikakati yake. Wengine wanahofu kuwa, hatimaye mradi huu utahamishiwa eneo la Delta ya mto Pearl. For example, “ocean_Joe” alisema:

:凡事要三思而行。zf为何会引进该项目?为何不在咨询广大民众后才考虑引进?为何要在13日内决定一项可能会影响几百年甚至几千年嘅事?今日核息,明天会不会又有新花样?请不要触碰到广大江门以及珠三角人民的底线,珠三角是我家。

Ocean_Joe: Tunapaswa kuwaza kwa makini. Kwa nini serikali iliamua kuuleta mradi huu? Kwa nini haukutambulishwa mara baada ya kupata maoni ya wananchi? Kwa nini serikali ilidhamiria kufanya maamuzi yatakayoathiri maisha yetu na ya watoto wetu ndani ya siku 13 tuu? Mgogoro sasa umetulizwa, lakini ni nani anayejua ni lini na wapi mradi huu utaanzishwa tena katika siku zijazo? Tafadhali msijaribu kupima misimamo ya watu wa Jiangmen nay a wale wa Delta ya mto Pearl. Nyumbani kwangu ni huko kwenye Delta.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.