Wakazi wa Jiangmen Nchini China Wapinga Ujenzi wa Mtambo wa Uranium

Siku ya tarehe 12 Julai, 2013, mamia kadhaa ya wakazi wa Jiangmen, jiji lililo jirani na Guangzhou ya Kusini nchini China, walifurika mtaani kuandamana kupinga mpango wa kuanzisha mtambo wa kuchakata Uranium .

Waandamanaji walitembea maeneo mbalimbali ya jiji wakiwa wamebeba mabango pamoja na kuvaa mabarakoi yaliyo na maandishi yaliyoandikwa “tunataka watoto, siyo atomi”. Waanadamanaji wanasema kuwa wanahofia mionzi na uwezekano wa uchafuzi utakaosababishwa na mtambo huo wa nyuklia.

Kwa mujibu wa gazeti la The New York Times, serikali ya Jiangmen tayari imeshaweka mkataba na Shirika la Taifa la Nyuklia la China katika kufadhili mradi huu kwa kiasi cha dola bilioni sita za kimarekani. Ujenzi unatarajiwa kuanza mwisho wa mwaka huu. Serikali ya mtaa ilitangaza mradi huu wiki iliyopita na kuwapa wananchi siku kumi za kuwasilisha maoni yao. Pamoja na maafisa wa serikali kudai kuwa mradi huu hauna madhara, lakini wananchi bado hawajaridhika. Katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa baada ya maandamano, Meya wa jiji hilo aliahidi kuongeza muda wa siku 10 zaidi kwa wananchi kutoa maoni yao.

Mapema mwaka huu, maandamano kama haya yalifanyika huko Kunming ya Kusini nchini China ambapo wakazi wa huko waliandamana kupinga kujengwa kwa kiwanda cha kusafishia mafuta.

Gazeti la South China Morning Post lilitaarifu kuwa, maandamano yaliratibiwa kupitia mitandao ya kijamii ya nchini China ya huduma za ujumbe ambayo ni: QQ na WeChat.

Kwenye tovuti ya jukwaa la kublogu la Sina Weibo, taarifa kuhusu maandamano haya kwa haraka kabisa iliweza kuratibiwa. Baadhi ya watumiaji wa Weibo waliweza kufuatilia taarifa hizo na na pia kuweka picha.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za maandamano kutoka Sina Weibo:

protest

jiangmen protest3

jiangmen protest

protest

protest

Bango linalosomeka: Tunataka watoto na siyo atomi. (Kutoka Sina Weibo)

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.