Kuelekea uchaguzi wa Kambodia: Matumizi ya Mtandao wa Facebook

Watumiaji wa mtandao wa intaneti nchini Kambodia wanatumia mtandao wa Facebook kwa kiwango kikubwa katika kujadili, kuendesha midahalo na kushirikishana mambo mapya yanayohusu chaguzi za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika tarehe 28 Julai, 2013. Wakati huohuo, vyama vya siasa pia vinatumia mtandao huu ulio maarufu zaidi katika kuwashawishi vijana wadogo wanaotarajiwa kupiga kura.

Moses Ngeth, ambaye ni mwanaharakati na wakili wa masuala ya haki za binadamu, alikiri kosa lake kufuatia tamko lake la hivi karibu kuwa, watumiaji wa Facebook nchini Kambodia wautumia mtandao huu kwa minajili ya burudani tu:

Miezi kadhaa iliyopita nilifanya mahojiano na vyombo vya habari na kusema kuwa, vijana wnatumia Facebook kwa ajili ya burudani tu na mambo yao binafsi. Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu, vijana wanaotumia mtandao wa Facebook walithibitisha kuwa mawazo yangu hayakuwa sahihi; na ni kweli ninakiri kuwa, tamko langu halikuwa sahihi. Nimeona idadi endelevu ya vijana wanaotumia Facebook kwa ajili ya kutafuta mabadiliko. Kwa wale vijana wote makini ambao wamesimama kidete na kwa uwazi katika kutumia haki yao ya kumchagua kiongozi wao, ninawaomba msamaha

Princess Norodom Arunrasmey, daughter of late king Norodom Sihanouk and head of the royalist party, cheers her supporters gathered at the Freedom Park in Phnom Penh. Photo by  Thomas Cristofoletti, Copyright @Demotix (7/3/2013)

Malkia Norodom Arunrasmey, ambaye ni mtoto wa hayati Mfalme Norodom Sihanouk na kiongozi wa chama cha Kifalme akiwapungia mkono wafuasi wake waliokusanyika katika Bustani ya Uhuru (Freedom Park) huko Phnom Penh. Picha naThomas Cristofoletti, Copyright @Demotix (7/3/2013)

Rachna Im, ambaye ni mwandishi wa habari wa RFI katika lugha ya Khmer na ambaye ni mwanablogu chipukizi mwanamke alikubaliana na Moses katika ujumbe alioujibu na kwa kuutuma kwa mwandishi wa makala hii:

Mtandao wa Facebook umekuwa ukitumiwa kwa namna mpya na ya kipekee kabisa. Watumiaji na hususani vijana, siku za hivi karibuni wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kama nmna ya kutolea maoni yao yanayohusu siasa. Kama nilivyobaini, hii ni namna nzuri ya kutumia mitandao ya kijamii-katika kuhakikisha mawazo ya mtu yanasikika na pia inaonesha hali nzuri ya uhuru wa kujieleza nchini Kambodia, siyo sana, lakini kwa kiasi fulani, hali inaridhisha..

Hata vivyo, Rachna aliwakumbushas watumiaji wa mtandao wa intaneti wanaoshiriki kwenye midahalo ya kisiasa kuheshimu hali ya mgongano wa mawazo:

Mara nyingi huwa wanaishia kuwatukana wengine pale kunapotokea mgongano wa kimawazo. Wanaamini kuwa wana uhuru wa kukiunga mkono chama fulani-lakini hawaheshimu haki ya watu wengine ya kukiunga mkono chama kingine. Wakati mwingine huwa ninashangazwa sana na baadhhi ya mambo yanayowekwa kwenye Facebook, kwani huwa ninajiuliza kitu hicho kimewekwa tu bila hata ya kutumia akili.

Zaidi, Rachna aliwapongeza vijana kwa basara zao katika kutoa maoni yao na kuamini kuwa utaratibu huu utaiimarisha jamii na haswa haswa katika suala la uhuru wa kujieleza nchini Kambodia.

Chantra Be, msimamizi wa mfumo mtandao wa kijamii wa Asasi Huru na mtaalamu wa kuratibu matukio ya BarCamp huko Cambodia na ambaye anajulikana kwa kutokupenda kuzungumzia masuala ya siasa, siku za hivi karibuni alianzisha mjadala wa kisiasa. Katika maojiano na mwandishi wa makala hii, Chantra alielezea ni kwa nini kwa ghafla alihamasika kwenye mambo ya siasa:

Binafsi sipendi siasa, na mimi siyo mwanachama wa chama chochote. Ninapenda kuwa vuguvugu. Mimi ni raia niliye na haki ya kupiga kura na kutoa maoni yangu. Nimesoma mambo mengi kuhusiana na hali ya sasa ya Kambodia katika mtandao wa Facebook yaliyonigusa.

Hivi karibuni, Chantra alihoji jukumu la washauri 164 wa chama kilicho madarakani kama wameshaishauri kwa makini serikali katika mambo fulani kama vile ya afya, elimu, mahakama, uwekezaji na mali asili.

Screen shot 2013-07-10 at 12.37.03 PM

Sovichet Tep, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya upili na miongoni mwa wanablogu wadogo kabisa nchini Cambodia, pia, aligundua hali ya kuongezeka kwa umuhimu wa uanahabari wa kijamii nchini mwake:

[…] ការចែករំលែកព័ត៌មានជាច្រើននៅលើបណ្ដាញសង្គម មិនមែនទើបតែកើតមានឡើងស្របពេលជិតបោះឆ្នោតឡើយ […] បើតាមខ្ញុំចាំគឺប្រហែលនៅពាក់កណ្ដាល ឬ ចុងឆ្នាំ២០១១ អ្នកប្រើប្រាស់បណ្ដាញសង្គមហ្វេសប៊ុកចាប់ផ្ដើមប្រែប្រួល ដោយផ្ដោតលើការចែករំលែកព័ត៌មាន ព្រោះព័ត៌មានមួយចំនួនពុំត្រូវបានចាក់ផ្សាយពេញលេញតាមបណ្ដាញផ្សព្វផ្សាយដូចជាទូរទស្សន៍ឬវិទ្យុឡើយ។

[…] upashanaji wa habari umekuwa wa haraka sana sito tu mara baada ya kuanza kwa chaguzi[…]. Kwa kumbukumbu zangu, utaratibu huu ulianza tangu katikati au mwisho wa mwaka 2011 pale watumiaji wa Facebook walipoanza kupashana habari ambazo watu hawakuwa wakizipata kupitia vyombo vya habari vilivyozoeleka kama vile televisheni na na redio. blockquote>
Pamoja na kuwa Sovichet bado hajafikia umri wa kupiga kura, anaamini kuwa, utaratibu wa kupashana habari kupitia mtandao wa intaneti utamsaidi kufikia maamuzi sahihi kwa uchaguzi unaofuata:

ថ្វីបើខ្ញុំពុំទាន់គ្រប់អាយុបោះឆ្នោតក្ដី (តែនឹងចូលរួមក្នុងអាណត្តិក្រោយមិនឲ្យខាន) ក៏បណ្ដាញសង្គមលើអ៊ីនធឺណិតនោះ បានបង្ហាញឲ្យខ្ញុំយល់ជាក់ច្បាស់អំពីស្ថានការណ៍នាពេលបច្ចុប្បន្ន ដើម្បីត្រៀមខ្លួនដើម្បីជ្រើសរើសគណបក្សមួយដែលខ្ញុំគិត និងសង្ឃឹមថាធ្វើបានប្រសើរសម្រាប់ប្រទេសជាតិ។

Pamoja na kuwa mimi bado ni mdogo kiasi cha kushindwa kupiga kura (lakini nimeshakuwa na maamuzi sahihi ya kupiga kura kwenye uchaguzi unaofuata), mitandao ya kijamii kwa hakika imenifundisha mengi kuhusiana na hali ya kisiasa iliyopo hivi sasa na hivyo kuweza kujiandaa kuchagua chama ambacho ninafikiri na kuamini kuwa kitakuwa na manufaa kwa jamii yetu.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.