Habari kuhusu Kambodia

Ramani Hizi Zaonesha Mahali Walipotesewa na Kuuawa Wanahabari wa Kambodia

  2 Juni 2015

Kituo cha Haki za Binadamu cha kambodia kimezindua jarida linaloelezea ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa kwa waandishi wa habari nchini Kambodia. Katiba ya nchini Kambodia inatoa uhuru wa kupashana habari lakini wanahabari wanazidi kunyanyaswa na kuuawa, hususani kwa waandishi wanaopasha habari kuhusiana na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na maafisa...

Udhalilishaji wa Kijinsia wa Watoto Wanaotalii Asia ya Mashariki

  4 Julai 2014

Mradi wa Nguzo ya Kuokoa Utoto, uliobuniwa na serikali ya Australia, umezinduautafitiukosefu wa msaada wa kijamii, elimu, furasa na ulinzi” kwa kuendelea kwa vitendo vya kuwadhalilisha watoto. Utafiti huo pia umeonyesha namna kusafiri na utalii “ni hatari nyingine inayochangia shida za kudhalilishwa zinazowakumba watoto.” Utafiti huo ulihusisha nchi za Thailand,...

Magonjwa ya Afya ya Akili Hayapewi Kipaumbele Nchini Cambodia

  28 Aprili 2014

Akiandika kwa niaba ya Southeast Asia Globe, Denise Hruby aliripoti jinsi wagonjwa wa akili katika maeneo mengi ya vijijini vya Cambodia wanavyofanyiwa: …Wagonjwa wa akili bado hutibiwa na waganga wa jadi, ambao lengo lao ni kuwatoa pepo wabaya kwa kuchoma ngozi, au kwa wafanyakazi wasio na ujuzi wa chumba kimoja...

Kwa nini Maandamano Hayatasababisha ‘Mapinduzi ya Cambodia’

  4 Machi 2014

Faine Greenwood anaandika kuhusu mhadhara wa Stanford uliotolewa na mwanaharakati wa haki za binadamu wa Cambodia Ou Virak. Aliuliza kuhusu maandamano ya kupinga serikali yanayoendelea nchini Cambodia, Ou Virak alieleza kwa nini hayatasababisha ‘mapinduzi ya kisiasa': Sidhani kuwa mapinduzi ya Cambondia yatatokea, na wala sidhani yanahitajika…Hatuna hata neno muafaka kwa...

Jinsi Vyombo vya Habari vya Kijamii Vimeleta Mabadiliko ya Kisiasa Nchini Cambodia

  8 Novemba 2013

Colin Meyn anaelezea jinsi ‘kuenea kwa haraka kwa kwa vyombo vya habari vya kijamii kunabadilisha mazingira ya kisiasa nchini Cambodia.’ Vijana wapiga kura wanaotaka mabadiliko pamoja na kampeni ya fujo ya upinzani katika mtandao ulifanya athari kubwa katika uchaguzi wa hivi karibuni. Jambo la kushangaza, Waziri Mkuu pia alitaja Facebook...

Hali ya Uislamu Katika Asia ya Kusini

  27 Julai 2013

Murray Hunter wa Chuo Kikuu cha Malaysia Perlis anajadili hali ya jamii ya Kiislamu katika Asia ya Kusini pamoja na masuala yanayohusiana na kukua kwa Uislamu katika eneo hilo. Umaskini, kujua kusoma na kuandika, elimu, kuhamishwa, ukabaila, ukosefu wa ajira, ukandamizaji, na udhibiti ni mambo yanayowaonea Waislamu ndani ya ASEAN. Serikali pamoja na...