Taarifa ya Raia Mtandaoni: Sheria Mpya Cambodia na Tanzania Zimelazimu Vyombo vya Habari vya Kujitegemea Kuwa Kimya au — Kufungwa

Kibanda cha kuuzia Gazeti la Citizen, gazeti la kujitegemea Dar Es Salaam, Tanzania. Picha na Adam Jones kupitia Wikimedia Commons (CC BY-SA 3.0)

Taarifa ya raia mtandaoni ya Advox inaangazia taswira ya kimataifa juu ya changamoto, ushindi na mienendo inayoibuka katika haki za kimtandao duniani.

Wakati uchaguzi ukikaribia mwezi ujao wa Julai kamati ya uchaguzi ya taifa Cambodia imetangaza mipango kadhaa inayotarajiwa kudhibiti habari mtandaoni .

Kikundi kipya cha kazi baina ya wizara kiliundwa kuchunguza vyombo vya habari vinavyosambaza “habari za uongo”, kimetoa sheria mpya ambayo inawafungia waandishi wa habari kama watatoa “habari za chuki au maoni yao” katika kuhabarisha, kuchapisha habari ambazo zinaathiri, “utulivu wa kisiasa na kijamii”, kuendesha mahojiano kwenye vituo vya kupigia kura au kutangaza habari “ambayo inachochea vurugu au kupoteza kujiamini” katika uchaguzi. Uvunjaji wa sheria adhabu yake ni faini ya dola za kimarekeni 7,355.

Wizara ya habari itawezeshwa kufanya sensa ya tovuti na mitandao ya kijamii zitakazokuwa zinavunja sheria. Watoa huduma za mtandaoni watatakiwa kufunga programu ambayo itaiwezesha wizara ya posta na mawasiliano “kuchuja kirahisi au kuzuia tovuti yoyote, akaunti au kurasa za mitandao ya kijamii ambazo ni haramu”.

Hatua hizi zimepelekea magazeti ya taifa mawili pekee ya kujitegemea kusitisha huduma – Gazeti la Phnom Pehn Post na la kila siku la Cambodia. Baada ya kupokea bili ya kodi kubwa, gazeti la Daily lilisimamisha shughuli zake mwezi Septemba 2017, wakati mmilki alipoliuza. Sasa machapisho yanamilikiwa na Sivakumar s Ganapathy ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ASIA PR ya Malaysia ambayo inafanya kazi kwa niaba ya chama tawala na waziri mkuu Hun Sen wa Cambodia.

Wakati huo, “kodi mbaya ya wanablogu” Tanzania itaanza kutumika tarehe 15 mwezi Juni na wanablogu na wamilki wa tovuti watahitajika kujiandikisha na kulipa kiasi kipatacho dola za kimarekani 900 hivi kwa mwaka ili kuweza kuchapisha habari mtandaoni.

Blogu na aina nyingine za maudhui matandaoni kama vile You Tube zitakazofanya kazi baada ya tarehe 15 Juni bila ya leseni, zitapigwa faini “isiyo chini ya shilingi za kitanzania milioni tano” (sawa na dola za kimarekani 2,500),au kifungo “cha miezi sio chini ya 12 au vyote.”

Vituo vingi vikubwa vya magazeti vimefunga maduka , vikidai kuwa gharama ni kubwa – kiuchumi na kisheria kwa pamoja. Jamii Forums ambayo ni mashuhuri sana — ambayo imepewa majina ya “Reddit ya Tanzania” na “Wikileaks ya kiswahili” — limefunga shughuli zake wiki iliyopita kwa sababu ya sheria ina vikwazo kwa vituo kama cha Jamii Forums. Mwezi Desemba 2016, jeshi la polisi Tanzania lilimkamata Maxence Melo, mwanzilishi na Mkurugenzi wa Jamii Forums kwa kukataa kutoa taarifa ya wanachama wake agizo lililotolewa chini ya sheria ya uhalifu mtandaoni .

Umoja wa waandishi wasiokuwa na mipaka umeomba serikali kurekebisha sheria hiyo mpya.

Mwanaharakati na mwandishi wa kujitegemea Bangladeshi auawa mbele ya umma

Mwandishi wa kujitegemea Bangladeshi, Shahzahan Bachchu alipigwa risasi na kuuawa karibu na mji wa Munshiganj anamoishi. Bachchu alijulikana sana kama mwanaharakati anayetetea dini isiwe msingi wa utawala, na alichapisha shairi na vitabu juu ya ubinadamu na mawazo huru. Alilipotiwa kuwa ameburuzwa nje kidogo ya duka la dawa na kupigwa risasi na waendesha pikipiki.

Kifo cha Bachchu kinafuatia mfululizo wa kuvamiwa wanaharakati wa haki za binadamu na wenye mawazo huru katika Bangladesh pamoja na kuuawa waandishi na mwakili wa digitali kama Avijit Roy, Washiqur Rahman, Ananto Bijoy Das, Niloy Neel na wengine. siku za nyuma, maafisa wa serikali akiwemo waziri mkuu Sheikh Hasina walilaumu kuvamiwa kwa wanaokufuru Mungu kwa kukosoa dini.

Mwanabloga Mualjeria afungwa miaka 10 kwa sababu ya mahojiano ya video

Mwanabloga ambaye ni mualjeria Merzoug Touati alifungwa miaka kumi jela mwishoni mwa mwezi Mei kwa kutoa habari mtandaoni juu ya mgomo mkali, kugoma kazini na uvunjaji wa haki za binadamu. Touati ambaye amekuwa jela tangu Januari 2017 anashtakiwa kwa kutoa taarifa za “kiintelejensia kwa wakala wa nchi moja ya nje ili idhuru jeshi la Algeria au uwezo wa kidiplomasia au faida ya kiuchumi” baada ya kutuma mtandaoni mahojiano na afisa wa Israel. Touati anatarajia kukata rufaa kwa hukumu hiyo.

Mtumiaji wa facebook alikamatwa kwa kulaumu miundombinu mibovu

Mtu mmoja kutoka Kerala India, alikamatwa na polisi baada ya kuandika kwenye Facebook kuhusu barabara iliyoharibika na kuomba mwanasiasa aikarabati. Mwanasiasa alidai kuwa taarifa ile ni “kashifa” na kwamba ametukana jinsia na dini yake. Aliwasilisha malalamiko polisi ambao bila kuchelewa walimkata. Muda mfupi baadaye mtu huyo alitolewa kwa thamana.

Mwandishi wa habari mrusi alilazimika kujihuzuru kutokana na maoni yake kupitia Instagram

Mwandishi wa habari Mrusi Alexandra Terikova alilazimika kujihuzuru kwa kutuma kwenye Instagram video ya wanafunzi wa chekechea wakiimba wimbo kuusu Rais Vladimir Putin na kisha akatoa mahojiano na chombo cha habari kimoja cha kujitegemea. Video ile ilitumwa pamoja na alama ya kejeli na ujumbe mkali wa sauti ya wimbo na wa shari.

< Hukumu ya kifo na video ya kirusi vinaweka alama ya mwisho ya matumizi ya telegramu katika Iran

Muirani mwanaume anakabiliwa na adhabu ya kifo kwa kutuma kupitia kituo cha telegramu ambacho kinaruhusu watumiaji kutuma maoni yao kwa uhuru kabisa. Hamidreza Amini atakwenda mahakamani tarehe 25 Juni kwa mashtaka ya “kumtukana nabii”, “kumtukana kiongozi mkuu ”, “kuhatarisha usalama wa taifa”, “propaganda za kupinga nchi” na “kuvuruga maoni ya umma”.

Amini alishikiliwa na kuhojiwa bila kupata ushauri wa kisheria baada ya kukamatwa. Kituo cha haki za binadamu cha Irani kililipoti kuwa Tarehe 3 Juni Amini alianza kugoma kula akishinikiza kuhudumiwa na alipelekwa hospitali na kulazwa lakini kabla hajakamilisha matibabu kamili alirudishwa gerezani.

Mahakama yaIrani iliamuru tarehe 30 Aprili telegramu zizimwe kwa sababu ya usalama wa taifa. Tangu hapo wimbo wa kubeza unaohusu kuchuja kwa telegramu na kundi la muziki ya bendi ya Dasandaz ya Irani ulivuma kwenye mitandao ya kijamiii ikichochea kuicheka serikali kwa kujaribu kuwaandalia wairani jukwaa la Soroush la kutuma ujumbe linalomilikiwa na nchi.

Vituo vinavyoongoza kwa habari Venezuela vimefungwa

Vituo viwili vya habari ambavyo vimeweza kuripoti juu ya migogoro ya kisiasa na kiuchumi inayoendelea tangu miaka minne iliyopitavimeondolewa kwenye mtandao kutoka kwenye huduma ya mtandao mkubwa wa taifa wiki ya kwanza ya Juni. Ushahidi usio rasmi na wa kiufundi unathibitisha kuwa Patlila na El Natiocional zilikuwa hazipatikani kwenye CANTV ambayo ndiyo kituo kikubwa cha nchi kinachoongozwa na mamlaka ya nchi ambacho hutoa huduma ya mawasiliano.

Kufungwa huko kunatokana na tamko la mahakama la El Nacional kupigwa faini ya bilion moja fedha ya Venezuela (sawa na dola za kimarekani 10,000) kutokana na madai ya serikali kwamba gazeti hilo limesababisha “uharibifu wa maadili ” kwa chama cha kisoshalisti (PSUV) cha Venezuela na makamu wa Rais Diosdado Cabello alipokuwa kwenye majumu yake kama Rais wa Bunge la taifa.

Tovuti ya chama cha siasa Pakistani yafungwa

Kuelekea uchaguzi wa tarehe 25 mwezi Julai, tovuti ya chama cha siasa kinachojulikana kama chama cha wafanyakazi Awami ilifungwa katika Pakistani kwa siku tatu hivi. Ingawa waliiandikia tume ya uchaguzi na Mamlaka ya mawasiliano ya Pakistani (ambay ndiyo inayowajibika kufunga), viongozi wa chama hawajapewa maelezo yoyote juu ya kufungwa huko.

Mahakama ya uchaguzi Brazili emeanzisha sheria ya habari za uongo

Tarehe 7 Juni, mahakama kuu ya uchaguzi Brazil (TSE) iliamuru Facebook kuondoa “habari za uongo kuhusu mgombea [Urais] Marina Silva” ndani ya masaa 48 baada ya hukumu. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa amri ya mahakama baada ya kutolewa mwaka 2017 ikihusu maamuzi yanayoazimia kupunguza kuenea kwa habari za uongo kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2018.

Mahakama ilimpa ushindi mgombea Urais na chama chake cha Rede ambacho kilihoji taarifa tano zilizotumwa na ukurasa wa right wing zikidai Silva alikuwa anachunguzwa na kampuni ya kuosha gari ya Operation, kwa ajili ya utakatishaji wa fedha ambao ulihusisha wabrazili 100, maofisa wa mafuta na wanasiasa. Kumekuwa hakuna mashtaka rasmi kwa Silva juu ya rushwa. Ukurusa mpya huo unawafuasi wapatao milioni 1.7.

Je, Ufaransa itatunga sheria ya habari za uongo?

Bunge la Ufaransa lilianza kujadili mswaada wa serikali unaolenga kuzuia “habari za kutengeneza” kwa miezi mitatu kabla ya uchaguzi. Sheria itawaruhusu wagombea kulalamikia habari za uongo juu yao zilizoenezwa mtandaoni na mahakama itafanya maamuzi ndani ya masaa 48. Tarehe 7 Juni wakati wa kipindi cha majadiliano, wabunge wa upinzani wa mlengo wa kulia na kushoto walifunga mjadala wa mswaada huo.

Tafiti mpya

 

 

Jiunge na taarifa za raia mtandaoni

 

 

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.