Habari Kuu kuhusu Korea Kusini
Habari kuhusu Korea Kusini
Mkimbizi na Mchora Vibonzo wa Korea Kaskazini Achora Kuhusu Maisha Yalivyo Kwa Watu Wanaotoroka
Akiwa mtoto, walimu walimsifu Choi Seong-guk kwa michoro yake ya wanajeshi wa Kimarekani ambapo anasema aliwafanya waonekane "wabaya na wakatili kadri ilivyowezekana."
Korea Kaskazini: Ni Lini Itaanguka?
Ingawa Korea Kusini inaonekana kutengeneza mahusiano na Korea ya Kaskazini, wataalamu wana wasiwasi kidogo kuhusu kubashiri kuanguka kwa Korea Kaskazini. NKnews.org ilichapisha posti nzuri kuhusu uwezekano wa kutawanyika kwa utawala wa kidikteta, akihitimisha kuwa ‘mageuzi ya kiuchumi ya Pyongyang yanaongeza uwezekano wa tukio la kuanguka vibaya’.
Mazungumzo ya GV: Tafakuri ya Kina Kuhusu Muziki wa Mahadhi ya Pop Nchini Korea
Umekuwa ukiitwa “bidhaa kuu ya mauzo nje” ya taifa la Korea Kusini. Wimbo wa PSY ulio katika mahadhi ya Pop ndio wimbo uliotazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube. Lakini nyuma ya hali hii inayoonekana kijuu juu kuwa ni kupendwa na malipo makubwa kadhalika, muziki huu hauwezi kuwa mzuri wala wa...
Picha Mpya ya Korea Kaskazini ya Shirika la Anga la Marekani
Wasomaji wa kimataifa wanaofuatilia masuala ya Korea Kaskazini labda wangekutana angalau mara moja na picha hii maarufu ya rasi ya Korea kutoka Shirika la Anga la Marekani (NASA) kuonesha tofauti kubwa ya taa zinazoangaza usiku kwenye nchi hizo mbili za Korea. NASA hatimaye walihuisha picha zao za Satelaiti na ‘ina mwonekano mzuri kuliko picha ya...
PICHA: Vyama vya Wafanyakazi na Asasi za Kiraia Vyaandaa Mgomo
Huku ukiwa umepangiliwa ufanyike mwanzo wa kipindi cha pili cha Rais Park Geun-hye madarakani, takribani wa-Korea elfu 40 (polisi wanadai ni elfu 15) walifanya mgomo nchini kote. Mgomo huo, ulipangwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Korea, ukiwa na wito wa kusitishwa kwa kudhibitiwa kwa vyama vya wafanyakazi, hatua...
Rais wa Korea Kusini Aapa Kupambana Uzushi Unaoenezwa katika Mitandao ya Kijamii
Je, serikali ya Korea Kusini imejiandaa kwa kufuatilia mitandao ya kijamii? Matamshi ya hivi karibuni ya Rais Park (full transcript [ko]) yamewashitua wa-Korea wanaotumia mtandao. Park, akiwalenga “uvumi ule unaosambaa kupitia mitandao ya kijamii”, alisema “kama serikali ikiachia mambo haya yakaendelea, itakuwa ghasia nchi nzima” na kuongeza “kumbukeni mamlaka za nchi zinahitaji...
Korea Kusini: Mwandishi Msafiri, Utamaduni Tofauti, na Jamii ya Wageni
John Bocskay, mwanablogu asiyeandika mara nyingi sana alifanya mahojiano na mwandishi wa utalii Rolf Potts aliyetumia miaka kadhaa kwenye jiji la pili kwa ukubwa nchini Korea Kusini, Pusan, anasema: Kila mtu niliyeonana naye katika vilabu vya wageni alidai kuwa mwandishi au msanii, lakini hungeweza kuona maandishi mengi au sanaa. Ilikuwa...
South Korea: Ahadi ya Rais ya Ustawi Iliyoshindwa Yakosolewa
Rais Park yuko kwenye wakati mgumu kwa r ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni kuwa angepandisha ruzuku ya pensheni gharama za mafunzo. Wakosoaji wanasema kampeni yake iliahidi kinyume na sera yake kama mgombea mhafidhina, ilimsaidia kuzoa kura katika uchaguzi uliopita. Akaunti ya mtandao wa twita wa @metempirics ilikusanya viunganishi vinavyohusika na...
Korea Kusini: Mpango wa Kuwakutanisha Wenzi Wakwama
Mpango mpya kabisa wa kuwakutanisha wenzi kwa njia rahisi katika mkesha wa Krismas nchini Korea Kusini hatimaye ulijikuta ukishindwa kabisa baada ya waliojitokeza asilimia 90 kuwa ni wanaume. Inasemekana zaidi ya watu 20,000 walijiandikisha na hata polisi walikuwepo kufuatia uwezekano wa vitendo vya ngono za kulazimisha. Mtumiaji mmoja wa mtandaoalibainisha [ko]...
Korea ya Kusini: Mabadiliko ya Sheria kuhusu Uzazi wa Mpango Yaibua Mjadala Mkali
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya nchini Korea imetangaza kwamba dawa za kuzuia mimba za dharura zinazofahamika kama 'morning-after pills' zitaanza kupatikana kwa wingi. Hata hivyo, dawa za kuzuia mimba zisizo za dharura zimekuwa dawa za kuandikwa na daktari. Mabadiliko haya ya ghafla kuhusu dawa za kuzuia kuzaliana limeibua mjadala mkubwa mtandaoni.