Ni “Udhaifu” wa Serikali, Yasema Ripoti ya Ajali ya Kivuko cha Korea Kusini

Yellow Ribbons tied by citizens, hoping for miracles, at one random street of Seoul, Image by author.

Utepe wa njano ukiwa umefungwa katika mtaa wa Seoul kwa matarajio ya muujiza wa janga la kivuko cha Sewol. Picha na Lee Yoo Eun.

Zimetimia siku 14 tangu kivuko cha Korea Kusini kizame kikiwa na abiria mamia kadhaa. Mpaka sasa, watu wapatao 205 wamethibitishwa kupoteza maisha, na wnegine 97 bado hawajulikani walipo.

Nahodha na wafanyakazi wote wa kivuko wote wamewekwa ndani. Waziri Mkuu Chung Hong-won tayari amejiuzulu kufuatia serikali kushutumiwa kuwa ilichelewa kuchukua hatua kukabiliana na janga hilo. Watu watatu kutoka kwenye ofisi ya Incheon ya Chama cha Usafiri wa Majini cha Korea nao wamekamatwa kwa tuhuma za kuharibu ushahidi.  

Wakati taarifa zaidi kuhusu uzembe wa serikali ya Korea Kusini katika kushughulikia ajali hiyo  zimepatikana, hasira za wananchi zimeendelea kuongezeka. 

Kwenye mtandao, watumiaji wa intaneti wamezilaumu mamlaka za serikali na vyombo vya habari kwa kuendelea ‘kuimba’ visingizio vinavyotolewa na serikali: 

Mbinu mbovu za kukabiliana na majanga, udhaifu na uongo, na vyombo vya habari vinavyoendelea kudanganya mfululizo…Yote haya yameziumiza familia. Katika ajali hii ya kivuko cha Sewol, udhaifu wa serikali hii umefunuliwa.

Rais haonekani kwenye taarifa za habari. Madudu ya idara za serikali na makosa mengi na kushindwa kwa serikali havionekani kwenye taarifa za habari. Kama ilivyotokea kwenye kuzama kwa kivuko cha Sewol, nahodha wa meli alikimbia. 

Vyombo vya habari vinaonyesha video inayoonesha vifaa vilivyookolewa kutoka kwenye eneo la ajali ya kivuko hicho na vipande vya video zilizotengenezwa na wataalamu wakati wa zoezi la ukoaji. Inaonekana zoezi hilo linaendelea kwa ufanisi -kama tunategemea kupata habari kupitia vyombo vya habari pekee. Hata hivyo, hakuna wahanga wengine ukiacha wale waliokuwa wameokolewa katika eneo la ajali. Hakuna maendeleo, lakini vyombo vya habari vinaendelea kupiga porojo. Eneo hasa ilikotokea ajali ni tofauti na lile linaloonyeshwa na vyombo vya habari.

Hasira imechochewa zaidi na wanasiasa wanaoonekana kutumia tukio hilo kisiasa.

Mbunge wa chama tawala cha Saeunri yuko kikaangoni kwa kumtuhumu kimakosa mzazi wa mmoja wa wahanga wa ajali hiyo [ko] kuwa mtu asiyehusika ‘anayetaka kuchochea tu hasira dhidi ya serikali’. Mbunge huyo baadae alieleza kwamba alikuwa amepotoshwa na picha bandia zilizokuwa zinasambaa mtandaoni.  

Polizi hivi sasa wanamchunguza mwandishi  [ko] aliyeandika kwenye mtandao wa Facebook kwamba “Janga la kivuko cha Sewol ni tukio lililotengenezwa na vibaraka wa Korea Kaskazini wanaotaka kutengeneza mazingira ya hali ya sintofahamu na tahayaruki katika jamii ya Korea Kusini. ” 

Sasa mbinu za kuwaita watu “wakomusnisti wekundu” na “Vibaraka wa [Korea] Kaskazini” limekuwa jambo la kawaida siku hizi. Hali hii inaudhi sana. Kila mmoja anamtuhumu mwenzake kuwa ni “Kibaraka wa kaskazini” au “Shushushu wa Korea Kaskazini” kila panapokuwa na hali ya kutokuelewana. Watu wale ambao bado hawajakata tamaa na zoezi la uokoaji linaloendelea, watu hao ambao wako katika wakati mgumu wanaweza kuumizwa kirahisi na matamshi ya namna hiyo. Tuangalie kile tunachokisema.

Wakati nchi yote imezizima na kukata tamaa na kukaongezeka sauti za watu wanaoikosoa serikali, chama tawala na wafuasi wake wameanza kutengeneza propaganda ya “Vibaraka wa Kaskazini”. Mazingira haya yamenifanya vifikiri kuhusu kile kilichoifanya nchi yetu iingie kwenye matatizo. Kama hatuwezi kubadili uongozi unaofunika udhaifu wake kwa mbinu za eti ‘Ukibaraka wa Kaskazini’, basi hatuna jawabu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.