Korea ya Kusini: Mabadiliko ya Sheria kuhusu Uzazi wa Mpango Yaibua Mjadala Mkali

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Korea ilitangaza mnamo tarehe 7 mwezi Mei, 2012,kuwa dawa za kupanga uzazi za dharura zinazojulikana kama dawa za mara baada ya kujamiiana (morning-after pills) zitaanza kununuliwa bila hata ya kupata ushauri wa daktari. Hata hivyo, mabadiliko haya yamesababisha dawa zisizo za dharura za kupanga uzazi [ambazo hapo awali zilitumiwa bila ulazima wa ushauri wa daktari] kuhitaji kwanza ushauri wa daktari kabla ya kutumiwa. Pamoja na hayo, ushauri wa kitaalamu kuhusu njia za uzazi wa mpango za dharura kwa vijana umeonekana kuwa bado utahitajika.

Mabadiliko haya ya ghafla kuhusiana na kanuni zinazoongoza matumizi ya dawa, yameibua mijadala mikali katika mtandao. Wakati bado kukiwa na mijadala endelevukuhusiana na madhara na manufaa ya njia hii ya dharura ya kuzuia mimba miongoni mwa watabibu, watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti wa Korea wamekwishaonesha kutoridhishwa na mabadiliko haya. Kama ilivyokaririwa katika gazeti la Hangyoreh [ko]mashirika ya kutetea haki za wanawake na haswa wanawake vijana ambao hawajaolewa, yamekwishapinga uamuzi huu kwa kuwa gharama za dawa za kuzuia mimba zilizopendekezwa haziendani na hali halisi.

Contraceptive pill. Image by Flickr user  Beppie K (CC BY-NC-SA 2.0).

Vidonge vya kuzuia mimba. Picha na Flickr user Beppie K (CC BY-NC-SA 2.0).

Mtumiaji wa Twita, @redparco aliwakumbusha [ko] wale wasiokubaliana na suala la wanawake wa jamii ya watu wa Korea ya Kusini ambao hawajaolewa [wanaoenda kwa wataalamu wa kitabibu wa magonjwa ya wanawake] kuwa ni watu wasiotaka mabadiliko na ni wa mfumo dume. Mtumiaji huyu wa twita alisema;

유럽은 다들 그렇게 하고 있다는 얘길 하려면 한국에서도 그 나라들처럼 부인과 진료나 사전,사후 피임약의 접근성이 좋아져야지. 한국 미혼 여성들이 사전 피임약 처방 받으러 산부인과 자연스럽게 드나들 수 있는 분위기나 마련하고 할 말이지.

Wanapotaka [Mamlaka ya Usimamizi wa Chakula na Dawa] kufananisha na hali ilivyo Ulaya, basi wanapaswa kwanza kuhakikisha kuwa kuna huduma za kutosha za wataalamu wa magonjwa ya wanawake na upatikanaji mzuri wa dawa za kupanga uzazi kama inavyofanyika katika nchi hizo za ulaya. Angalao wanapaswa kuandaa mazingira ambayo yatawafanya wanawake wa Korea kuwa huru kuonana na wataalamu wa magonjwa ya wanawake ili kupata ushauri kuhusiana na dawa za kuzuia mimba za kumeza”.

@marisusa came up [ko] alikuwa na wazo linalofanana na la mchangiaji aliyetangulia. Alisema::

[…] 사후피임약이라는 단어 뉘앙스가 피임책임을 여성 일방에게만 지우는 방식으로 악용될 우려가

“Dawa za dharura za uzazi wa mpango ni kama kuwalaumu wanawake kwa kile kilichotokea. Na kuna dalili kuwa zingalikuwepo dharau za namna hiyo”.

ThinkThink,baada ya kualika watumiaji wengine wa mtandao katika mjadala, aligundua [ko] kuwa kubadilika ghafla kwa sheria hii kumechochewa na kutaka faida kubwa zaidi kuliko kuthamini huduma za afya kwa jamii. Shin Jae-eun alitoa mawazo yake kufuatia mawazo ya mtumiaji mwingine wa mtandao. Alisema:

병원처방이 필요해지면 남의 눈 의식하다보니 못가기도 할꺼고 피임률은 줄고 오히려 낙태률이 높아질듯 싶네요[…]진짜 적극 반대네요.

“ Wakati ambapo dawa za kumeza za mpango wa uzazi zinapokuwa ni lazima kwanza kupata ushauri wa wataalamu kabla ya kutumia, watu walio na woga haitakuwa rahisi kwao kuonana na wataalamu [wa magonjwa ya wanawake] ambapo hali hii inaweza kusababisha kuongezeka kwa matukio ya utoaji mimba na hatimaye kuzuia mimba likawa jambo lililoshindikana. Binafsi sikubaliani na mpango huu kabisa.

Wakati watumiaji wengi wa mtandao wakionya kuhusu madhara ya dawa za kupanga uzazi za dharura, wakati mwingine wakizitafsiri kama ‘dawa hatari kwa homoni.’, Mtumiaji mmoja wa Twita @__mangmang alisema [ko]:

사후피임약은 그야말로 ‘응급'피임약이고, 일반의약품으로 전환되는 건 옳다고 생각한다. 그러나 경구피임약(사전 복용)이 전문의약품화되면 10대들, 작은 공동체에 사는 비수도권 여성들의 피임약 구매는 현실적으로 더 어려워질 거다.

“Dawa za muda mfupi za kupanga uzazi, kama jina lenyewe linavyotanabaisha ni kidonge cha “dharura”, kwa hiyo hakuna ubaya kwa utaratibu huu wa kununua bila hata ya ushauri wa daktari. Hata hivyo, ikiwa dawa za kumeza za uzazi wa mpango zitakuwa katika mfumo wa kuhitaji kwanza ushauri wa daktari, haitakuwa rahisi na haitowezekana kabisa kwa vijana na wanawake wanaoishi nje ya miji na wale wa jamii ya hali ya chini kununua kidonge [bila mashaka yoyote]

Mbali na makundi ya kutetea haki za wanawake, Kanisa Katoliki nalo linapinga uamuzi huu. Kanisa Katoliki katika jimbo la Chungcheong waliitisha maandamano mbele ya jengo la Mamlaka ya Chakula na Dawa wakionya kuwa [dawa za dharura za kuzuia mimba] vidonge hivi vinaweza kuathiri imani za watu na kuwapa mafundisho ya kuwapotosha kuhusiana na thamani ya maisha hususani kwa vijana- mtazamo ambao watumiaji wengi wa twita hawautilii maanani

@symadam5 alisema [ko]:

사후피임약 일반의약품 판매로 성문란,낙태조장을 주장하는 가톨릭은 […] 현실감각이 없는건지,이 나라 불법낙태와 해외입양율 보면 이미 최고수준인데 왠 상상력?사전피임못함 사후라도 해야니 긴급,응급피임약인데 72시간내 먹는게 낙태란건 과장이 심해

Hao wakatoliki wanaodai kuwa dawa za dharura za kupanga uzazi kuweza kutumiwa bila ya kupata ushauri wa daktari kunaweza kuhamasisha kupotea kwa maadili na kuhamasisha utoaji mimba- wameshindwa kuupata uhalisia? Kiwango cha utoaji mimba ambao si halali tayari upo juu sana katika nchi hii na hata kimataifa. Wana fikra zisizo na mashiko kwa kiasi gani? Kama mtu akishindwa kutumia njia ya kumeza vidonge vya kuzuia mimba, basi hana budi kutumia vinginevyo – na hii ndio maana inaitwa njia ya kupanga uzazi ya “dharura”. Ni upotoshaji kusema kuwa kutumia kidonge cha uzazi wa mpango ndani ya saa 72 kuwa ni utoaji mimba

Sera hii mpya ya njia za uzazi wa mpango inategemewa kuanza kutumika rasmi mapema mwaka ujao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.