Feri ya Korea Kusini iliyokuwa inaelekea kwenye kisiwa cha mapumziko ilizama mnamo Aprili 16, 2014 na mamia ya abiria, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 325 wa shule ya sekondari waliokuwemo. Zimetimia siku mbili tangu ajali hiyo itokee na watu 28 wamethibitika kufariki kufikia Aprili 18 na watu 268 bado hawajulikani walipo. Uwezekano wa kupona ni mdogo mno.
Picha tatu hapa chini zimetolewa hadharani kupitia ukurasa wa Facebook wa Coast Guard [ko]. Picha ya kwanza inaonyesha nahodha wa mashua akiwa miongoni mwa kundi la kwanza kuokolewa.
Mijadala ya mtandaoni nchini Korea Kusini imefurika salamu za rambirambi kwa waathirika na wapendwa wao pamoja na hasira kali dhidi ya nahodha na wafanyakazi ambao waliokolewa mapema zaidi kabla ya abiria. Kilichochochea hasira zaidi ni tangazo linalosemekana kutolewa kwenye feri hiyo kuwaambia abiria waendelee kubaki ndani [ko], hata wakati feri ilipoanza kuzama.
#Sewol 2003년 대구지하철 방화 참사 때 기관사가 마스터키 뽑고 도망가는 바람에 승객 다수가 사망했습니다. 세월호 선장과 기관사 등의 조기탈출 이야기가 들립니다. 부디 사실 아니길 바랍니다. 사실이라면, 처벌은 당연하고 결코 용서받지 못합니다.
— … (@DrPyo) Aprili 16, 2014
Mwaka 2003 wakati wa maafa ya moto ya reli ya chini ya ardhi ya Daegu, idadi kubwa ya abiria walikufa wakati kondakta wa treni alikimbia baada ya kukwanyua ufunguo. Mimi nasikia masimulizi kuwa nahodha wa feri ya Sewol na kondakta waliokolewa mapema. Ningependa iwe ni uongo mtupu. Kama hiyo ni kweli, basi hawawezi kusamehewa wala kuepuka adhabu.
선장이 가만히 있으라는 방송을 말단 여직원에게 시키고 본인은 1차로 탈출했다는 소식을 들으니 옛날 한국전쟁때 이승만이 이젠 안전하다는 방송을 하고서 한강다리 끊고 도망갔다는 이야기가 떠오른다. 무려 60년이 지났는데도 어쩜 이렇게 그대로인지…
— 풋비홀릭 (@FootvieHolic) April 16, 2014
Nahodha, baada ya kuagiza mfanyakazi wa kike wa ngazi ya chini kutangaza kwamba abiria wanatakiwa kukaa mahali walipo, alitoroka vizuri kabla ya mtu mwingine yeyote. Inanikumbusha tukio la kihistoria wakati wa Vita vya Korea – wakati Rais Rhee Seung-man, baada ya kutangaza kwamba “sasa hali ni shwari”, walikimbia baada ya kukata daraja mto Han. Imekuwa ni zaidi ya miaka 60, lakini historia inajirudia.
Mamlaka bado haijaweza kuthibitisha nini kilichosababisha tukio hilo, na uvumi mbalimbali imeibuka, ikiwa ni pamoja na feri inaweza kuwa iligonga mwamba. Hivi sasa, wengi wanatoa lawama kwamba meli ilifanyiwa utengenezaji kinyume cha sheria[ko] ili kuwabeba abiria zaidi. Watumiaji mtandao Korea wakijadili siri ambazo hazijatatuliwa.
세월호 의문점들 1. 기상 좋고 암초 없는 곳에서 조난 2. 선체 우측 바닥에 움푹 패인 자국 3. 침수 중 “가만 있으라” 방송 4. 선장과 선원 먼저 탈출 5. 조난신고를 승객 가족이 8시 58분에 함 6. 지역 어민은 7시 30분 경 세월호 발견
— ㅂㄴㅂ (@yimoha) April 16, 2014
Kuna maswali yaliyobaki: 1) jinsi gani feri ilizama katika eneo hilo na hakuna mwamba na hali ya hewa ilikuwa nzuri siku hiyo 2) Upande wa kulia wa sehemu kuu ya Feri kumebonyea sana. 3) Tangazo la “kaeni mlipo” wakati meli ilianza kuzama4) wafanyakazi na nahodha kuokolewa kwanza 5) wito wa dhiki ulifanywa saa 8:58 na abiria 6) mvuvi mdogo kuona kuna kitu kisicho sawa na Sewol saa 7:30.
Wengi walilaumu hisia na kuchukulia urahisi kupitia kwa vyombo vya habari.
문화일보 초판을 보면 얼마나 나태하게 여객선 세월호 침몰을 대했는지를 알수있습니다. MBC는 구조작업이 끝나기도 전에 돈얘기를 합니다. KBS는 생존자나 구조소식보다 대통령동정이 더 중요합니다. (아이엠피터) pic.twitter.com/fAOWSjnBSK
— 서영석#국민TV라디오 (@du0280) April 17, 2014
Kama ukiangalia ripoti ya awali ya gazeti la Munhwa, unaweza kuona jinsi walikuwa wavivu katika kuripoti suala hili. Mazungumzo MBC kuhusu fedha za [bima] hata kabla ya operesheni ya kuwaokoa kumalizika. KBS inalenga zaidi juu ya majibu ya rais kuliko waathirika na taarifa juu ya ujumbe wa kuwaokoa (kupitia mwanabloglu kwenye mtandao kupitia alama ashiria “Mimi ni Peter”)
Ujumbe wa kuwaokoa unaendelea. Hata hivyo, jamaa na familia ya waathirika walitoa taarifa [ko] kukemea kwamba bado hakuna taarifa zinazoeleweka pamoja na habari za kutiwa chumvi kuhusu ukubwa wa timu ya waokoaji.
도착시간 5시 30분쯤 진도 실내체육관 비상상황실에 와보니 책임을 가지고 상황을 정확히 판단해주는 관계자가 아무도 없었습니다다. 심지어 상황실도 없었습니다다.[…] 어제 현장을 방문했습니다. 인원은 200명도 안됐고, 헬기는 단 두대. 배는 군함 두척. 경비정 2척. 특수부대 보트 6대. 민간구조대원 8명이 구조작업 했습니다다. 9시 대한민국 재난본부에서는 인원 투입 555명. 헬기 121대. 배 169척으로 우리아이들을 구출하고 있다고 거짓말 했습니다.
Tulipofika saa 5:30 katika ukumbi wa michezo wa Jindo ambapo ni kituo cha dharura, hakukuwa na mfanyakazi ambaye alikuwa na wajibu wa kuwaambia watu nini kinaendelea. Hakukuwa hata na kituo cha udhibiti […] Sisi tulitembelea eneo la ajali jana. Timu ya kuwaokoa ilikuwa chini ya watu 200 Kulikuwa na helikopta mbili tu, mashua mbili baharini, mashua mbili za walinzi wa pwani, mashua sita ya vikosi maalum.. Na watu wanane wa timu ya uokoaji wamefanya zoezi la kuokoa. Hata hivyo, Makao Makuu ya maafa yamesema uongo kwetu sisi kwamba wao waliwapeleka wanachama 555 wa uokoaji, helikopta 121 na mashua 169.
**Ripoti zaidi itafuatilia kuhusu maafa.